Tuweke utani Pembeni, Soka la Yanga ni tamu jamani

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Mtangazaji Mpenja akazidi kulinadi soka lile kwa kusema linapendeza unaliangalia huku ukitupia bisi moja moja mdomoni!

Nilikaa jirani na mashabiki baadhi wa timu ya upande mwingine tena baadhi yao wakiwa na jezi zao yaani wametulia tulii hawakutoa maoni yeyote lkn nadhani nao pia wameburudika sana jioni ya jana!

Taifa kwa sasa halipati burudani nyingine tamu ya soka popote pale zaidi ya Yanga ichezapo na hili halina ubishi maana tafiti zisizo rasmi zimeonyesha siku yanga inacheza mashabiki wengi wa soka huenda uwanjani au hukusanyika katika pubs,hotels,mabanda umiza na majumbani wakifuatilia mtanange...hakuna timu nyingine inayothubutu ...

Hongera sana wachezaji na benchi lote la ufundi kwa uwajibikaji wenu mnaotuonyesha,taifa linasubiri burudani zingine siku ya jumanne na pia siku ya sikukuu jumapili..huku tukiwasubiri hao Us Monastry tuje tuwashikishe adabu kama ndugu zao.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Kweli mnacheza vizuri,lakini kwa nini mnapenda kufanya maigizo?

Mara kadhaa mwamuzi anawabeba na bado tunaona wachezaji wa timu pinzani wanafurahia ushindi wenu

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Maigizo yapi? kwa nini mnapenda kulalamika kiasi hiki? mnataka mfungwe nyie tu? Kuna wakati mnaboa mno! Mbona simba akishinda hamtowi hizi kauli? Kwa hiyo maigizo yalishindikana kwa Ihefu? Hivi kweli Yanga hawezi kuifunga Polisi ( iliyofungwa na timu kibao) mpaka yafanyike maigizo!?
 
Kweli mnacheza vizuri,lakini kwa nini mnapenda kufanya maigizo?

Mara kadhaa mwamuzi anawabeba na bado tunaona wachezaji wa timu pinzani wanafurahia ushindi wenu

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Wewe jamaa huna ubongo Bali kichwa chako kimejaa kinyesi Cha vyoo vya stand ya Magufuli,sijui ndy umeandika Nini hiki

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Safi sana umejibu vizuri sana hasa kwenye bold.

Hakuna haja ya kujipakulia minyaaaaaama na mnajua ni vibonde, team nyiiingii zimejibondea tu.
 
Kama ni maigizo basi hata wao huwa wanafurahia ushindi wa Yanga

Kwanini,
Kuanzia msimu wa 2020_2021 hadileo hii tunawadunda tu
Katika mashindano ambayo lazima mshindi apatikane, kama ngao ya hisani FA Simba hafui dafu kwa Yanga.

Sanasana sare ndiyo ushindi wake
 
Kweli mnacheza vizuri,lakini kwa nini mnapenda kufanya maigizo?

Mara kadhaa mwamuzi anawabeba na bado tunaona wachezaji wa timu pinzani wanafurahia ushindi wenu

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Na nyie mmezidi kwa gubu khaaa,mmekuwa kama wake wenza, kwaiyo mnawaonea gubu polisi kupewa kichapo mnataka nyie tu ndio muwe mnagongeshwa peke yenu? Acheni mambo ya ovyo basi kila timu itapewa stahiki yake ipasavyo msijali ya kwenu iko njiani
 
Ukweli kabisa yanga ndio team yenye mashabiki wengi Africa mashariki ile siku wanacheza na club africain uwanja ulijaaa mpaka wengine wakakosa pakukaa na wengine walibaki nje baada ya kukosa ticket kweli ujinga mzigo yaani unajisifu kwa mechi za bahasha kweli na ulozi wa kuvaa jezi nyeusi subirini mashindano ya wanaume Caf confederation cup huko ndio kutatoa majibu yote.
 
Dah watu wanaumiaa
 
Kweli mnacheza vizuri,lakini kwa nini mnapenda kufanya maigizo?

Mara kadhaa mwamuzi anawabeba na bado tunaona wachezaji wa timu pinzani wanafurahia ushindi wenu

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Wivu tu kama mke wa kwanza. Mnataka mfungwe nyie tu na Yanga wakifungwa wengine mnanung'unika
 
Wivu wa nini?subiri zamu yako ifike ntakuja kula.la huko kwako,sasa ivi ni zamu ya wenzako.
 
Wivu tu kama mke wa kwanza. Mnataka mfungwe nyie tu na Yanga wakifungwa wengine mnanung'unika
Wanawake wa kingoni wana wivu sana,kama vip tff waisogeze karibu game tuwape wanachotaka
 
Kwani jana kulikua na mechi ya Yanga??
Alicheza na nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…