Hawa diplomasia ambao hawajui chochote kuhusu mambo ya Fedha kuwapa majukumu ya kujua kila kitu kuhusu pesa na budget zao ni tatizo. Hiyo ingetakiwa kuwa kazi ya watu wengine na inawezekana kabisa serikali ingetoa kazi hii kwa chombo kimoja badala ya kuwapa kazi ambazo hawaziwezi. Yaani kuwa balozi sio lazima uwe na CPA. Raisi Samia anaongea kama vile hawa si wazalendo.
Kitendo cha kuwapa majukumu ya kuwa kama CPA ni zaidi ya uwezo wa diplomasia wengi na kwa mwenendo huu tutabaki na CPAs kama mabalozi badala ya wana diplomasia. Hawa diplomasia hawajui lolote kuhusu CAG.
Inasemekana balozi wetu umoja wa mataifa kafukuzwa kwasababu ubalozi umetumia pesa vibaya lakini ni vigumu kwa balozi kufanya kazi ya ubalozi na kufuatilia matumizi ya pesa za balozi. Hii kazi ya kufuatilia pesa na matumizi ingepewa kitengo maalumu na sio wanadiplomasia wetu