Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Hamu kubwa ya kupata maarifa na ufahamu wa mambo ni jambo lililofanya mataifa ya ulaya kukua.
Bila maarifa hakuna jamii itakayopiga hatua kimaendeleo. Jamii yeyote itakapoanza kuheshimu maarifa na kuyatafuta kwa hali na mali, ili kuendesha maisha yao ya kila siku, Jamii hiyo ni lazima itaendelea.
Ujinga ndio kitu kinachorudisha nyuma mataifa mengi na kuyafanya yasiendelee. Na hatua moja kubwa na muhimu kwa taifa lolote kuendelea ni kupambana na ujinga. Na kukuza ufahamu wa watu wake.
Ni watu ndio wanaoleta maendeleo katika nchi. Hata tuwe na maliasili kiasi gani lakini kama hatuna watu waliopevuka kiakili maliasili hizo hazotowasaidia.
Kwahiyo ni muhimu kwetu kuwekeza katika watu. Kwasababu watu wetu wasipokuwa na ufahamu wa kutosha maliasili zetru hazitowasaidia, zitawasaidia watu wenye maarifa na utaalamu.
Tungekuwa na maarifa na utaalamu , maliasili zetu zingetusaidia zaidi ya ilivyo sasa, hasa kwenye gesi na madini yetu. Tuna maarifa madogo sana na ni wajibu wetu kukuza ufahamu wetu katika mambo mbali mbali.
Sisi ni taifa dhaifu kwasababu hatuna maarifa ya kutosha. Na pengine hatujisumbui vya kutosha kuyatafuta.
Wenzetu Ulaya na Marekani wamefikia mbali sana na hata Asia. Sisi kazi yetu kununua kila kitu kilichotokana na uwezo wa kufikiri na kugundua wa wenzetu.
Lakini tujue kwamba wote tuna ubongo sawa ni jinsi gani tu tunavyoelekeza mawazo yetu.
Akili zetu kama waafrika , tunazielekeza katika nini na tunazitumiaje? hiki ndio kitu kinacho tutofautisha sisi na wao.
Kama tutachukua muda wetu mwingi kufikiri ni jinsi gani tutakabiliana na matatizo yanayotukabili tutapiga hatua.. Na uhakika muda si mrefu taifa hili watu watalisahau kama Tuwekeze katika maarifa ya watu wetu.
Kitu muhimu ni uwepo wa nia ya kutaka kuona taifa hili likiendelea na kupiga hatua na kubadilisha watu wake kutoka katika ujinga, maradhi na umaskini.
Adui yetu mkubwa ni ujinga, ni mkubwa kuliko hivyo vingine viwili , kwasababu watu wetu wakiwa na maarifa wataondokana na umaskini na maradhi kwa kiasi kikubwa. Tutashinda maradhi na ujinga kwa kuelimisha watu wetu.
Ni lengo la Taifa lolote kujenga jamii yenye afya na yenye furaha. Lengo hili litafikiwa tu ikiwa watu wetu wakiwa na afya ya akili ya kutosha.
Wakiwa na ufahamu wa kutosha na wenye uwezo wa kuchagua yaliyo sahihi kwa Taifa lao, jamii zao, familia zao na kwao binafsi.
Mara nyingi furaha ya binadamu huondoka kutokana na chaguzi tunazofanya katika maisha. Kutokana na muelekeo tunaochagua katika maisha yetu iwe kama taifa au kama mtu binafsi.
Tunapochagua muelekeo wa haki na wa kutenda yaliyosahihi; matokeo yake lazima yawe yenye matunda mazuri. Kuliko tukichagua ubinafsi .
Ni lazima tujue ni vitu gani tuna ''values most'' katika maisha yetu kama taifa na kama mtu mmoja mmoja. Our Families, our nation or communities.
Kwahiyo ni lazima watu waangalie communities zao na taifa lao kuliko maslahi yao binafsi kama tunataka kujenga taifa lenye afya na furaha, lakini lenye ustawi wa kisiasa na kiuchumi.