Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
KILA mtu ana haki ya kuwa na familia. Hakuna apaswaye kumsumbua mwingine kwa namna yoyote.
Mungu ametuleta duniani tuzae ili tuongezeke, lakini hakututuma tuzae bila mpango ili tuwategemee wengine.
Kumbukumbu zangu za maandiko ya Biblia zinanieleza kuwa alisema asiyefanya kazi na asile ingawa hakukataza ndugu kusaidiana.
Hakusema tuzae na kuwatupia wengine jukumu la malezi bora ya watoto wetu, wala hakusema tuwazae na kuwatawanya bila uangalizi.
Anasisitiza wajibu wa wazazi kwa watoto wao na ndivyo hata Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano inavyoelekeza kuhusu haki yao ya kupewa chakula, mavazi na malazi bora.
Kadhalika, elimu bora japo ya msingi na maisha ya furaha ni wajibu wa wazazi pia. Cha kushangaza, kumekuwa na tabia ya watu wenye akili timamu kuzaa idadi kubwa ya watoto huku wakijua kuwa hawana uwezo wa kuwalea na kutupa majukumu yao kwa Serikali au watu wengine.
Watu hao, kwa sababu mbalimbali ikiwamo ya kutokuwa na Ukimwi, kuendeleza mila zilizopitwa na wakati, sifa, ujinga na ile ya Mungu kasema tuzaane, wamekuwa chanzo kikubwa cha Taifa lenye watoto wengi tegemezi wanaoishi kwa mateso na shida utadhani waliomba waletwe duniani.
Kama haitoshi, wapo wenye kudai eti wamezaa wengi kwa bahati mbaya, wengine wanajifariji kwa kusema ajali kazini au muujiza wa Mungu.
Huu ni ujinga kwa sababu si kweli, kwamba bahati hiyo mbaya na ajali zake itamjia mtu huyo huyo mara ya sita, ya saba, nane . Miaka ya enzi za wazazi wetu hii ilikuwa sawa, hali iliruhusu. Nasema hivyo, kwa sababu hali ya maisha ya sasa ni ngumu kwa wengi wetu na hairuhusu idadi kubwa ya watoto.
Aidha, kutokana na ugumu huo, inasababisha mateso makubwa kwa wazazi wenyewe na watoto wao licha ya kujikausha kwao kama hayawagongi. Ni kujifariji tu sababu mapato hayawiani na matumizi.
Utashangaa mama wa nyumbani asiye na mradi wowote na mumewe mpiga debe asiye na uhakika wa kipato, wanazaa zaidi ya watoto watano na kuwashangaa wenye mtoto mmoja, wawili au watatu na kipato kizuri kulingana na elimu zao za juu kutozaa kama yeye.
Ufike wakati tukome kubebwa na utumwa wa mila zilizopitwa na wakati na tukatae kufanya mambo bila kufikiria athari za baadaye. Hili hutokea na kama halijakukuta wewe basi limemkuta yule.
Ukiachilia mbali ombaomba wanaozaana kando kando ya barabara na kwenye vichochoro, wapo wenye akili zao timamu na uwezo wa kupanga vyumba vya bei ndogo, labda viwili vyenye umeme na maji ya wizi, wanasumbua wengine kwa kuomba malazi usiku kwa ajili ya baadhi ya watoto wao.
Maisha ya mijini hayataki familia kubwa kama huna uwezo. Unaweza kujisahau na kudhani vya watu ni vyako kwa kuwa ukiomba unapewa na hivyo kuendelea kuzaa. Tule kwa urefu wa kamba zetu.
Ni aibu, haina tofauti na ombaomba wanaojulikana, inaharibu starehe za wengine na kuwafanya waliozaa kwa mpango wabebe shida zisizo zao.
Ni kwa nini tusibadilike na kwenda na wakati? Ina maana watu bado ni mambumbumbu wa elimu ya Ukimwi?
Aliyesema ukizaa mtoto mmoja ndio umeathirika ni nani? Ni kwa nini tuwalete wakati hatuna hakika ya kula, kusoma na elimu yao? Aliyekwambieni Serikali inahusika na matunda ya starehe zenu ni nani?
Utasikia Serikali haijanisaidia ... ulivyomleta hukujua wajibu wako? Ninawazungumzia wanaoendekeza kuzaa na kuwashangaa wenye watoto mmoja mmoja au wawili kwa kuwa na idadi hiyo ndogo.
Unamkuta fukara asiyeweza kulisha watoto wake akimshangaa msomi mwenye mshahara wa zaidi ya kima cha chini kwa kuwa na mtoto mmoja na kumhisi kuwa huenda ana ngoma inayomzuia kuzaa.
Napata msukumo kwamba elimu ya Ukimwi iliyotolewa nchini haitoshi na kuwa mila potofu bado zinatesa watu. Usishangae kumsikia mzazi omba omba akiwashangaa wafadhili wake kwa kuwa na familia ndogo, tena wengine bila aibu wanauliza:
Una matatizo gani huongezi mwingine? Hujui unamkosea Mungu, nani kakwambia watakufa njaa? Uzazi wa mpango ni muhimu.