Tuzae kwa mpango ili tusisumbue wengine

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
KILA mtu ana haki ya kuwa na familia. Hakuna apaswaye kumsumbua mwingine kwa namna yoyote.

Mungu ametuleta duniani tuzae ili tuongezeke, lakini hakututuma tuzae bila mpango ili tuwategemee wengine.

Kumbukumbu zangu za maandiko ya Biblia zinanieleza kuwa alisema asiyefanya kazi na asile ingawa hakukataza ndugu kusaidiana.

Hakusema tuzae na kuwatupia wengine jukumu la malezi bora ya watoto wetu, wala hakusema tuwazae na kuwatawanya bila uangalizi.

Anasisitiza wajibu wa wazazi kwa watoto wao na ndivyo hata Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano inavyoelekeza kuhusu haki yao ya kupewa chakula, mavazi na malazi bora.

Kadhalika, elimu bora japo ya msingi na maisha ya furaha ni wajibu wa wazazi pia. Cha kushangaza, kumekuwa na tabia ya watu wenye akili timamu kuzaa idadi kubwa ya watoto huku wakijua kuwa hawana uwezo wa kuwalea na kutupa majukumu yao kwa Serikali au watu wengine.

Watu hao, kwa sababu mbalimbali ikiwamo ya “kutokuwa na Ukimwi”, kuendeleza mila zilizopitwa na wakati, sifa, ujinga na ile ya Mungu kasema tuzaane, wamekuwa chanzo kikubwa cha Taifa lenye watoto wengi tegemezi wanaoishi kwa mateso na shida utadhani waliomba waletwe duniani.

Kama haitoshi, wapo wenye kudai eti wamezaa wengi kwa bahati mbaya, wengine wanajifariji kwa kusema ‘ajali kazini’ au muujiza wa Mungu.

Huu ni ujinga kwa sababu si kweli, kwamba bahati hiyo mbaya na ajali zake itamjia mtu huyo huyo mara ya sita, ya saba, nane…. Miaka ya enzi za wazazi wetu hii ilikuwa sawa, hali iliruhusu. Nasema hivyo, kwa sababu hali ya maisha ya sasa ni ngumu kwa wengi wetu na hairuhusu idadi kubwa ya watoto.

Aidha, kutokana na ugumu huo, inasababisha mateso makubwa kwa wazazi wenyewe na watoto wao licha ya ‘kujikausha’ kwao kama hayawagongi. Ni kujifariji tu sababu mapato hayawiani na matumizi.

Utashangaa mama wa nyumbani asiye na mradi wowote na mumewe mpiga debe asiye na uhakika wa kipato, wanazaa zaidi ya watoto watano na kuwashangaa wenye mtoto mmoja, wawili au watatu na kipato kizuri kulingana na elimu zao za juu kutozaa kama yeye.

Ufike wakati tukome kubebwa na utumwa wa mila zilizopitwa na wakati na tukatae kufanya mambo bila kufikiria athari za baadaye. Hili hutokea na kama halijakukuta wewe basi limemkuta yule.

Ukiachilia mbali ombaomba wanaozaana kando kando ya barabara na kwenye vichochoro, wapo wenye akili zao timamu na uwezo wa kupanga vyumba vya bei ndogo, labda viwili vyenye umeme na maji ya wizi, wanasumbua wengine kwa kuomba malazi usiku kwa ajili ya baadhi ya watoto wao.

Maisha ya mijini hayataki familia kubwa kama huna uwezo. Unaweza kujisahau na kudhani vya watu ni vyako kwa kuwa ukiomba unapewa na hivyo kuendelea kuzaa. Tule kwa urefu wa kamba zetu.

Ni aibu, haina tofauti na ombaomba wanaojulikana, inaharibu starehe za wengine na kuwafanya waliozaa kwa mpango wabebe shida zisizo zao.

Ni kwa nini tusibadilike na kwenda na wakati? Ina maana watu bado ni mambumbumbu wa elimu ya Ukimwi?

Aliyesema ukizaa mtoto mmoja ndio umeathirika ni nani? Ni kwa nini tuwalete wakati hatuna hakika ya kula, kusoma na elimu yao? Aliyekwambieni Serikali inahusika na matunda ya starehe zenu ni nani?

Utasikia Serikali haijanisaidia ... ulivyomleta hukujua wajibu wako? Ninawazungumzia wanaoendekeza kuzaa na kuwashangaa wenye watoto mmoja mmoja au wawili kwa kuwa na idadi hiyo ndogo.

Unamkuta fukara asiyeweza kulisha watoto wake akimshangaa msomi mwenye mshahara wa zaidi ya kima cha chini kwa kuwa na mtoto mmoja na kumhisi kuwa huenda ana ‘ngoma’ inayomzuia kuzaa.

Napata msukumo kwamba elimu ya Ukimwi iliyotolewa nchini haitoshi na kuwa mila potofu bado zinatesa watu. Usishangae kumsikia mzazi omba omba akiwashangaa ‘wafadhili’ wake kwa kuwa na familia ndogo, tena wengine bila aibu wanauliza:

“Una matatizo gani huongezi mwingine? Hujui unamkosea Mungu, nani kakwambia watakufa njaa?” Uzazi wa mpango ni muhimu.
 
Kweli mwaya tena wengine hudiriki kusema mpaka mayai yaishe
 
Wengine wanasema wacha nizae tu kwani kila mtoto anakuja na riziki yake!
 
hapo umenena yaani unakuta mtu anazaa watoto kibao bila kufikiria namna ya kuwatunza matokeo yake anaposhindwa ada anaanza kuwahamisha nenda kwa mjomba,kwa kaka,kwa baba mkubwa na wakati huohuo hao relatives nao wana familia zao zinawashinda kulea!!!watanzania kweli mtindo huu inabidi tujirekebishe!
 
kama kawaida pdidy leo tena naona umegonga penye point. hii habari ya kubebeshana mizigo inatufanya tusiendelee. watu kila baada ya mwaka ana mimba huku hana mbele wala nyuma, mwingine hata mume hana utakuta kila mtoto na baba yake na waote analea mwenyewe, mi sipendi, nasema sipendi. Bora niwe na mtoto mmoja ambae nina uhakika wa kumtimizia mahitaji yote kuliko kuwa nao 7 ambao watakua machokoraa, yani useles kwa jamii maana hawana foundation yoyote ya elimu nk.
 
vp mkuu, hii january umelipa ada kwa wingi sana kwa ajili ya watoto wa ndugu mpaka wamekuboa? LOL
 
Hilo nalo neno kama watu wote tungekua na uelewa wa that level nafikiri jamii isingepata sana matatizo kwa kiasi cha sasa hivi!
 
Kuna Askofu huko Dodoma alisema kupanga uzazi ni dhambi, na kuwaasa waamini kuacha huo mpango mara moja.
 
Kuna Askofu huko Dodoma alisema kupanga uzazi ni dhambi, na kuwaasa waamini kuacha huo mpango mara moja.

basi na awasaidie kuwatunza na kuwasomesha. anasema ni dhambi mbona yeye hazai kabisa?
 

Tena hao hao utakuta wanakuteta eti wanajifanya wazungu, poa uzungu wangu ndio unaonifanya nimudu familia yangu na wewe kudhani nina ziada ya kukupa wewe, Pdidy hawa watu wanaboa sana kama sio kutuzeesha wenzao bila sababu
 
Natamani wangekusikia lkn bahati mbaya wengi kam asio wote hawafiki huku kabisaaaaaaa! labda tutunge wimbo tena wa taarab kwa ajili ya huu ujumbe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…