Pre GE2025 Tuzingatie nini katika kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Wabunge na Rais kwenye chaguzi zijazo?

Pre GE2025 Tuzingatie nini katika kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Wabunge na Rais kwenye chaguzi zijazo?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Pantosha

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
640
Reaction score
958
Viongozi tunaowachagua tunawapa mamlaka ya kutuamulia mustakabali wa maisha yetu katika kipindi chote cha uongozi wao. Viongozi hawa wanatunga sheria na sera kwa niaba ya wananchi wote, wanachukua mikopo kwa niaba ya watanzania wote, wanasimamia matumizi ya pato (uchumi) la taifa, ulinzi na usalama, elimu, afya, miundombinu,,ustawi wa wananchi kiumla.

Viongozi ni watu muhimu sana.

Katika kutambua umuhimu wao (viongozi), ni mambo gani ya kuzingatia tunapochagua viongozi katika ngazi tofauti tofauti?
Kuna mambo ya msingi sana yatatusaidia kupata viongozi watakao tusaidia kuleta maendeleo ya nchi.

Sifa zifuatazo zitatusaidia kuwachuja viongozi:

1. Utu:
Lazima kiongozi wetu ajali watu, awe na upendo, azingatie maadili yetu, sheria, taratibu tulizojiwekea, akubali kukosolewa, apokee ushauri, heshima kwa wengine, mpenda haki, mpenda Amani, nk

2. Mwenye maono
Lazima kiongozi awe na maono na lazima awe tayari anayafanyia kazi ili tuone kweli huyu ana maono hayo. Lazima ushahidi uwepo kuwa anatembea katika maono yake. Hatuhitaji mtu ambaye hajui anatoka wapi na anaenda wapi.

3. Azijue changamoto zetu na ajue namna ya kuzitatua.

4. Kwa nafasi ya rais lazima aijue nchi vizuri (historia), vyanzo vya mapato, ulinzi n.k.
Hatujitaji mtu ambaye hajui hata nchi inaenda je.

5. Mchapa kazi, mtu ambaye anapenda kusoma na uwezo wa kusoma kiswahili na kiingereza na kuelewa anachokisoma.

6. Anayezielewa siasa za dunia na namna ya kucheza nazo.
Hatutaki kiongozi ambaye haelewi kwamba tupo duniani na lazima kutangamana na watu wengine.

7. Uwezo wa kuongea/kuwasiliana vizuri

Wekeni sifa zingine
 
Viongozi tunaowachagua tunawapa mamlaka ya kutuamulia mustakabali wa maisha yetu katika kipindi chote cha uongozi wao. Viongozi hawa wanatunga sheria na sera kwa niaba ya wananchi wote, wanachukua mikopo kwa niaba ya

7. Uwezo wa kuongea/kuwasiliana vizuri

Wekeni sifa zingine
Hakuna hata kiongozi mmoja kutoka CHADEMA aliyekuwa na vigezo hivyo Juu, labda tukiongeza -Uharakati- labda.
 
Mustakabali wa maisha yako gani bhana,maisha yako pambania mwenyewe usitegemee lolote Toka Kwa wanasiasa,hao wenyewe wanagombea hizo nafasi kw ajili ya matumbo yao
 
Back
Top Bottom