Wazo zuri sana Mtanzania mwenzangu. Nadhani uzalendo huu upanuliwe na usiishie kwenye Taaluma tu. Unaweza kuongezea Michezo kwa Wanafunzi na mbinu mbalimbali za kuinua uchumi kwa Waalimu.
Mfano, Miaka michache iliyopita nikiwa Mkoa wa Shinyanga nilihamasisha na kuwajengea uwezo Waalimu wa Shule moja ya Sekondari hadi wakaanzisha Kikundi cha HISA kilichojumuisha baadhi ya Waalimu, baadhi ya Wafanykazi wasio Waalimu katika Shule hiyo na baadhi ya Wazazi. Mafanikio yalikuwa makubwa na mengi yakiwemo kupunguza kwa kiasi hulka ya Waalimu kukopa kwa "Loan Sharks" wa mitaani kwa dhamana ya Kadi zao za Benki, kuwawezesha Waalimu kufungua Miradi yao midogomidogo ikiwemo Kilimo na ufugaji wa Kuku, kuwaunganisha Waalimu na Wazazi na mwisho wa mwaka kugawana HISA na Faida iliyowawezesha baadhi yao kulipia Ada za Shule za Watoto wao. Mafanikio ya Kikundi hicho kwa Mwaka wa Kwanza yalisababisha kuundwa kwa Kikundi kingine hapo Shuleni. Leo ni Mwaka wa tatu, ninaamini wanaendela vizuri.
A happy Teacher is a Productive Teacher!
NB. Nilianzisha vilevile Kikundi kama hicho, cha HISA, kwa Manesi wa Hospitali ya Serikali.
Hivi sasa ninaishi kama viwanja/nyumba kumi kutoka Shule ya Msingi ya Serikali. Kutokana na wazo lako nitaonana na Mwalimu Mkuu tuone namna ninavyoweza kusaidia - kujitolea kwa masaa mawili kwa Wiki sio hasara.
Pamoja Tunaweza!