Tuzitunze timu zetu za mpira

ndunajr

Senior Member
Joined
Apr 28, 2015
Posts
174
Reaction score
191
Habarini wanajamvi,

Kichwa cha habari hapo juu ndicho kinabeba maneno yangu humu ndani. Ni kwamba Napata masikitiko makubwa sana juu ya hizi timu zetu hasa zinazoshiriki Ligi Kuu. Jana Simba na Majimaji zimecheza mechi ya mwisho katika mzunguko wa kwanza na timu yetu ya nyumbani Ruvuma na wanalizombe kutoka pale Songea mjini wakala nne bila; sikushangaa.

Maana yake siku tatu mpaka ile siku ya mechi walipangiwa kufikia Hotel moja hivi yaitwa Kilimanjaro ipo Tandika mtaa wa bububu aka Tandika maghorofani, hotel nzuri na kibwagizo tu ni sehemu ya machinjio ya wake za watu pale aah hatari.

Lakini kilichonistua mpaka kuandika hapa ni mtindo wa maisha wachezaji wanayoishi mmmhhhh aibu sana na ndo maana wachezaji wetu hawaheshimiki.

CHAKULA

Wachezaji wa Majimaji kwa siku tatu mfululizo walikuwa wanakula chakula cha mama Ntilie anaitwa Mama Mudy. Ni chakula ambacho mimi nilikula mara moja na kuapa Mungu nisaidie sitokula tena. Chakula nyama ajinamoto, wali hamira, kipande cha nyama kimoja dagaa kama watano mchicha daaa kiduuchu sahani bei 1500/=. Nami nina kaduka kangu ka soda na maji aahh wameniungishaaa. Sasa hebu niambie mimi tu kapuku msosi ule jinsi ulivyo kula mtihani halafu leo uwende ukawape wachezaji ambapo humo ndio ukatoe timu ya Taifa aaaaah samahanini jamani.

Nje ya Hotel sasa kuna duka sisi tunapaita Frem mpya bia zinauzwa hapo hatari eeeh bwana ule usiku kesho tunaamkia mechi ohoooo jamaa wanagonga monde hatari Jerryson Tegete anakula pombe hatari wamekunywa pombe wale watu hatari afu eti kesho unaingia uwanjani kucheza na Simba kwanini usifungwe?

Watu wakawa wanashangaa mabeki wanavyoanguka anguka tu uwanjani, kwa sisi tulioona yale maisha ndani ya siku tatu zile hatukushangaa wale wachezaji kukosa nguvu.

TUZITUNZE HIZI TIMU JAMANI, kweli chakula kwa MAMA MUDY!!!??? wadhamini wapo kweli???
 
Umenena vyema. Soka la tanzania linazidi kuzama, pamoja na mambo mengine, sababu ya ukata unaozikabili timu. Timu nyingi za kibongo hazina mifuko ya kutosha kujitegemea, au hata wadhamini wa kukidhi mahitaji ya timu. inafikia wachezaji wanacheza tu kwa sababu hawana sehemu ya kukimbilia.

viwango vya wachezaji vinayeyuka ghafla pale wanapokutana na mazingira magumu katika timu zao.TFF na Baraza la Michezo Tanzania wapo tu wanaganga njaa, hawana sera zozote kuwezesha angalau udhamini wa timu hizi ubalance na pengine kushurutisha wadhamini wa ligi na timu watimize mahitaji yote ya muhimu ya timu.

Wazamini wetu wamejikita katika kudhamini simba, yanga na Azam pekee, wakati timu hizi zina vyanzo vyake vya mapato tofauti na timu changa zingine. Wakongwe hadi leo wanategemea misaada ya wadhamini, miaka kibao wameshindwa kujiendesha wenyewe. ni aibu sana.

Ulaya timu zinafanya vizuri, sababu moja wapo ikiwa ni uwezo wa kiuchumi/kifedha. Ni ngumu sana kukomaa kisoka katika zama hizi bila kujijenga kifedha kwanza. Umaskini unawanyima wachezaji utulivu na concentration wakati wa mazoezi na mechi. umaskini unawafanya viongozi wa timu wafanye kazi kutokana na mashinikizo toka kwa wafadhili.

Tubadilike
 
Bongo kuna vipaji tatizo matunzo. Ni sawa na maofisi ya umma kuna watu vichwa sana ila mishahara ya aibu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…