Ndugu zangu je tunaweza kutengeneza vipeperushi zenye kuonyesha hali ya watoto wetu na kuvisambaza kwa watu wengi. Ndugu wa Kulikoni Ughaibuni je unatoa ruhusa watu tutumie picha zako na nyinginezo kuonyesha jinsi hali yetu ilivyo mbaya? Ninadhani vipeperushi ambavyo vina pucha kama hizi vitaisaidia kuwaelimisha Watanzania wenzetu kuweza kufanya uamuzi wa kweli. Yeyote mwenye takwimu nzuri katika huduma ya afya, elimu na maji zisaidia sana katika kuandika vipeperushi vya uhakika ili kuweza kuanika ukweli mbagani (hadharani) (Mimi hupenda kutumia maneno ya makabila yetu badala ya yale yenye asili ya kiarabu kama yapo kwani kanuni ya kwanza ya kutohoa Kiswahili ni kutumia neno la lugha yoyote ile ya kibantu kabla ya kutumia maneno ya nje ya lugha hizo. Kwa wenzetu Wahaya neno mbaga humaanisha umati wa watu na hivyo neno mbagani linafaa kwa malengo haya).