Tuzo ya Uandishi Zanzibar na Wabara waruhusiwe kushiriki

Tuzo ya Uandishi Zanzibar na Wabara waruhusiwe kushiriki

DustBin

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2021
Posts
609
Reaction score
604
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri,

Mimi ni katika waumini wa Muungano, na kawaida hua naupigia chapuo kutokana na manufaa yake kwa pande zote mbili.

Lakini hii ya leo imenifanya nishindwe kuvumilia hata kama nina kolomelo. Kuna kundi moja sogozi la waandishi nimeona kumetumwa tangazo la tuzo ya uandishi. Baada ya kusoma ndio nikajua katika masharti ya ushiriki wa tuzo hiyo sharti la kwanza lazima uwe Mzanzibar. Kilichonishangaza ni kwamba sisi tuna tuzo ya uandishi bunifu ya Mwalimu Nyerere, tuzo iliyoasisiwa na Profesa Mkenda (Waziri wa Elimu); inayosimamiwa na kuratibiwa na Taasisi ya Elimu (TET/TIE). Tuzo hii wanashiriki watanzania wote wa bara na visiwani. Ikiwa lengo ni kuvumbua vipaji na kuviendeleza, hasa waandishi chipukizi wa kazi za fasihi.

Ikiwa kama lengo ni hilo, kwa nini tuzo hii iliyotoleqa leo tangazo iwahusishe wa zanzibari peke yao??
Mbona ligi ya mapinduzi timu za bara zinashiriki?

Labda kuna kitu sikifahamu, naomba ueleweshqa tafadhali. Ila kwa maono yangu ingependeza hata hii tuzo ya uandishi Zanzibar ingetanua wigo kwa kuwaruhusu na waandishi wa bara, kwani wote tunajenga Tanzania moja.

Ndimi,
Mwana Muungano,
DustBin.
 
Sasa kama ni muumini wa muungano unahoji nini, badala ya kuendelea kupiga chapuo tu
 
Back
Top Bottom