Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Binadamu lazima akue na busara zake ziongezeke, tuzo ya umri mkubwa ni busara. Nje ya busara, kuwa na umri mkubwa bila maarifa ni upumbavu. Kama mto upelekavyo maji baharini na kujaza maji huko ndivyo binadamu anavyopaswa kuongeza maarifa yake na kujaza fikra zake na ufahamu.
Binadamu ni jinsi anavyofikiri, ni jinsi anavyoelekeza fikra zake. Ukielekeza fikra zako kwenye ujinga utarithi ujinga lakini ukielekeza fikra zako kwenye maarifa utarithi hekima.
Ni kama mtu shambani chini ya miembe, anaeokota maembe yaliyo mazima na kuyaweka kwenye kapu na kutupa yaliyo mabovu, na ndivyo ilivyo kwa binadamu na akili yake ni lazima achague mawazo yake na fikra zake zimwelekeze mahali bora na kuhifadhi kile kilicho bora katika ubongo wake na kuacha ujinga kwakuwa hauna manufaa. Ujinga ni adui wa mataifa, ni adui wa usalama na maendeleo ya watu.
Kwenye busara kuna matumaini lakini kwenye ujinga kuna kiza kinene, njia ya ujinga sio salama ni njia yenye kiza kinene lakini njia ya busara ni yenye kuelekea kwenye mwanga ni kuukaribia mwanga, ni kuukaribia mwanga mkubwa katika ukuu wake.
Kwa busara mataifa yalijengwa na kuimarishwa misingi yake, kwa maarifa yaliendelezwa. Kwenye busara kuna matumaini na furaha. Taifa lenye busara lina matumaini makubwa, lina kuridhika na furaha.
Kwanini wazee wapo, kama sio kuwa mfano kwa vijana na watoto wanaokua? kama sio kufundisha njia sahihi ya maisha yaliyo bora kwa vijana? wazee wanapokengeuka watakuwa na faida gani kwa jamii? je mwelekeo wa jamii na Taifa utakuwaje? Je tuzo ya umri mkubwa si busara? Wapo wapi viongozi wetu katika Taifa na katika jamii? Familia zinabomoka, mpangilio katika jamii unaondoka hakuna mashirikiano ya dhati na unafiki unatawala. Watoto wanakua kama uyoga bila maadili mema. Baadae ya Taifa letu ikoje? Umoja wetu, mwelekeo wetu! Taifa la wabinafsi hakuna dira ya pamoja kila mtu anajiangalia yeye. Utawala wa sheria umeondoka wanaua tembo, wanauza madawa ya kulevya kwa jamii yetu, tuna mwagiana tindikali yapo wapi mapenzi yetu?
mwelekeo wa Taifa letu utategemea sana busara na hekima zetu kuchagua njia iliyo sahihi kufanya mapito yetu kama Taifa. Lakini chumvi ya Taifa ambao ni wazee ikiharibika jamii hupotoka hadi hapo mche mpya uchipukie na kutoa matunda.
Pale serikali inapokuwa corrupt na inaposhindwa kutawala kwa sheria jamii ifanye nini? disorder huletwa na kutokuwepo na utawala wa haki.
Tumaini letu liko njia panda. Wale wanaotafuta uongozi wanatafuta kwa faida yao wenyewe na sio faida ya umma. We hope for God one day, he will install a leader to administer justice in his holy montain zion. Only by administration of justice we will bring order and direction to our country..then we will have a reason to hope for our future.