Tuzo za muziki za Kili

Paul S.S

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2009
Posts
6,407
Reaction score
3,260
Wadau jana ilikua ni siku ya kukabidhi tuzo za muziki za kilimanjaro. naomba mtu mwenye matokeo yalikuaje ayaweke humu tuyajadili
 
Zahir Ally Zoro....Hall of Fame

Banana Zorro ....Mwimbaji bora wa kiume

Twanga pepeta...Wimbo bora na Albamu bora ya bendi

Khalidi Chokoraa...Rapa bora

Bwana Misosi....Wimbo bora wa Ragga

Mrisho Mpoto....Wimbo bora wa asili

Mzee Yusuf....Albamu bora ya taarab

Lady JD....Mwanamziki bora wa kike

Diamond....Msanii bora anaechipukia, Wimbo bora wa R&B

AY....Wimbo bora wa Reggae

Marlaw....Wimbo bora wa Afro Pop

CPwaa...Video bora

AT....Wimbo bora wa kolabo ''Nipigie''
 
hii ragga na reggae hapa napata tabu saana, nikiona au kusikia nyimbo hizo, ma man tuko wapi!

Enh mwakani ntajitosa maana naona bado sijaguswa vilivyo katika anga hiyo ya midundo ya hisia na mikito ya kufa, mwagito mwagalinoma muko wapi? Nganyagwa, jhiko man, jet man, slim
daddy, na wengineo......................hapa kuna watu wanaonekana kulala.....................
 
Mwaka huu wamejirekebisha kidogo lakini bado
 
Lady JD Mwanamuziki Bora wa Kike........Ndizi Zoro Muimbaji bora wa kiume.Nadhani ipo tofauti hapo
 

Michuzi akitoa tuzo ya Hall of Fame kwa mkongwe Zahir Ally Zorro huku akishuhudiwa na wanawe Banana (kulia) na Maunda pamoja na mzee mzima Kassim Mapili (shoto)


Baba na mwana na familia wakifurahia tuzo zao ambapo baba kapata ya Hall of Fame na mwana kaibuka mwimbaji bora wa kiume kwa mara ya pili mfululizo


Mwenyekiti wa African Stars entertainment Baraka Msiilwa akiwa ameshikilia tuzo tatu ambazo Twanga Pepeta wamepata, ikiwa ni pamoja na wimbo bora, albamu bora ya bendi na rapa bora iliyoenda kwa Khalidi Chokoraa


Bwana Misosi akishangilia tuzo ya wimbo bora wa Ragga aliyopewa na Sean Kingston


Mrisho Mpoto (shoto) aliondoka na tuzo ya wimbo bora wa asili na 'Mjomba'



Mzee Yusuf Alikomba tuzo za albamu bora ya taarab na ya mtunzi bora


Gadna G. Habash akipokea toka kwa Tajiri Mpoki tuzo ya mwanamuziki bora wa kike ya Lady JD aliyopokea kwa niaba ya mai waifu wake Jide


Khalid Chokoraa akipokea tuzo ya Twanga pepeta wa Bendi bora


King Kikii akimkabidhi kwa Twanga Pepeta tuzo ya wimbo bora wa bendi


Lwiza Mbutu akisogea kutoa shukrani baada ya kupokea tuzo ya albamu bora ya bendi iliyoenda kwa Twanga Pepeta


Prodyuza bora wa mwaka akipokea tuzo



Diamond akisherehekea moja ya tuzo zake ikiwa ni pamoja na msanii bora anayechipukia, wimbo bora wa R& B toka kwa mwenyekiti wa Yanga Imani Madega


AY akisherehekea tuzo yake ya wimbo bora reggae


Lady JD akipozi na mai hazbendi wake na tuzo yake ya mwanamuziki bora wa kike


Marlaw akitamba na tuzo yake ya wimbo bora wa afro pop


Mwana FA na wenzake wakimtuza Diamond kwa kuwa msanii bora chipukizi


Hasheem Thabeet akimkabidhi C-Pwaaa tuzo ya video bora


Mwamvita Makamba na Ephraim Mafuru wakimkabidhi Banana Ally Zorro tuzo ya msanii bora wa kiume



Ras Inno Nganyagwa akimkabidhi AT tuzo ya wimbo bora wa kolabo aliofanya na Stara Thomas wa 'Nipigie'

Kwa msaada wa Michuzi Blog
 
Kuna wasanii kama AY,Lady Jay Dee,Banana kila mwaka lazima wapewe tuzo hata kama nyimbo zao mbovu
 
Michuzi nilikuwa nakusikia kwenye vyanzo mbalimbali vya habali ila kwa hayo mapicha ya KILI music Award nimekukubali! big up mkubwa.
 
Lilsun asante kwa habari hiyo,usikose leo diamond utupe majamboz kesho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…