Official Ric
Member
- Jun 20, 2024
- 31
- 75
Kuna uzi niliuandika namna gani kijana anayemaliza chuo anapaswa afanye ili aweze kuishi vizuri mtaani, nashukuru wanajukwaa kwa mwitikio wenu mzuri ila kuna baadhi ya wanajukwaa wansema kujitolea kwenye makampuni sawa ni wazo zuri kwa ajili ya kutengeneza CV yako, tatizo linakuja kuna baadhi ya makampuni kijana anajitolea anafanya kazi kwa moyo na Bidii lakin hakuna hata hela ya maji.
Uko unatoka nyumbani kwenda kazini lakini kila kitu kipo juu yako nauli utajigharamia chakula na bando yaani kila kitu ni juu yako utafikiri unafanya kazi za kanisa kumbe unafanya kazi kwenye kampuni ya mtu na unamtengenezea mtu faida.
Unajikuta unatumia mda mwingi kwenye kujitolea afu hupati kitu ata kama unapata basi ni kidogo sana hata hakikidhi mahitaji yako ya mwezi na Bado umri unazidi kusogea lakini labda hta ungeuza juice ya miwa ungetengeneza mara 2 au 3 ya ela unayoipata hapo kwenye hiyo kampuni na pia bado vijana wa kujitolea wanapitia mengi sana maofisini kama kutumwa chai na mabosi na kuwaoshea Magari.
Basi mimi ombi langu kwa wenye maofisi wawajali vijana wanaojitolea kwenye ofisi zao na pia sisi vijana tufanye kazi kwa biidi tuoneshe ufanisi wetu wa kazi na pia sisi kama wasomi tunafundishwa namna ya kutatua matatizo katika jamii, hivyo tuangalie tunasaidiaje vijana wanaomaliza vyuo au tunarekebishaje mitaala ili angalau kijana ajifunze ujuzi mbali mbali atakapo kuwa chuo ambao ni mbali na Field yake anayoisomea ili tumtengeneze kijana Bora katika Jamii.
Kwa Mfano kijana anayemaliza form six tunampeleka JKT miezi mitatu kwa nini tusingempeleka moja kwa moja Veta akapate ujuzi ambao utamsaidia yeye katika maisha yake au kijan baada ya kumaliza form 4 angeenda moja kwa moja VETA kabla ya kwend Form V au chuo.
Tungetengeneza vijana wapambanaji katika Jamii. Hayo ni maoni yangu vipi kuhus ww hapo mwanajukwaa ebu tujadili pamoja.