Tuzungumzie fursa zilipo maeneo yetu, mikoani na wilayani ulipo

WatesiWETU

Senior Member
Joined
Jan 2, 2022
Posts
106
Reaction score
248
Kuwa sehemu ya kuvutia wawekezaji katika wilaya au kata yako:

Wale wa mikoani wasaidieni hawa wa dar wajue fursa zilizopo mkoani kwako za kiasi cha mtaj wa kuanzia laki tano(500,000/=) mpaka milion moja(1,000,000/=)

Usiwe mchoyo wa mawazo naona vijana wengi wamemaliza vyuo ila wana banana hapa dar bila wazo na wengine wana laptop na simu za malaki ambapo wakiuza vyote hawakosi mtaji wa laki7 mpaka milioni moja .

Tatizo hawajui wafanyie nini wakisha ipata hiyo hela. Lengo la uzi huu nikutaka watu wa mikoani muwape mawazo ilinwaje kuzungusha mitaji yao uko.

Kumbuka , usipo kuwa mchoyo ukatoa wazo la biashara unayo ona inafanyika eneo lako huyu mtu akija uko atazidisha mzunguko wa hela na huenda mzunguko huo ukachangamsha mkoa wako au wiliya yako na hata mzunguko huo unaweza kukufikia hata wewe nakuchangamsha mapato yako binafsi.

Karibuni kwa shauri:
 
Korogwe , Tanga :

Kununua gunia la pumba ya mahindi Kijijini ( umbali wa kilomita 15 hadi 30 ), gharama yake ni 15,000/=

Guta linabeba gunia 10 ambayo ni sawa na Tsh 150,000. Usafiri wa guta kwa gunia 10 ni 10,000/=.


Korogwe Mjini pumba imesimamia 22 hadi 23,000/= kwa gunia moja la debe 7.

Kuna maisha hapo.

Mm nafanya hii project, lakini pia nasagisha na kukoboa. Nina mashine.
 
Sharing is caring[emoji4].

Shukran mkuu.
 
Tanga mjini au kipumbwi pangani au mkinga kuna fursa kubwa ya dagaa nyama ukitaka kuchemsha na kuuza au kununua na kuuza ni wewe tu dagaa hawa wanasoko sehemu yoyote ile ni watamu Sana kazi kwenu
 
Vip kuhusu gharama za mfuko na gharama za wapakiaji na washushaji.
 
Kizuri huko
 
nimepiga dili la cocoa kyela ipinda na matema, karanga tunduru msimu ujao jaribuni, ufuta nasubiri kulipwa ntawapa mrejesho nikilipwa
 
Vipi kuhusu upatikanaji wa wateja?
 
Badala ya ninyi kuanza kuchangia fursa zilizopo maeneo yenu, mnaanza kulaumu wabongo, ugonjwa wetu mkubwa sio uchoyo wa fursa, kwa sababu fursa huonekana na uhitaji kuambiwa zaidi ya kuitafuta, ugonjwa wetu ni lawama, kwa sababu lawama huangusha kulichosimama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…