Tuzungumzie Suala la Uchumi

Tuzungumzie Suala la Uchumi

Fundi Mchundo

Platinum Member
Joined
Nov 9, 2007
Posts
10,448
Reaction score
8,705
Marekani wana taasisi mbili ambazo naamini zingetusaidia sana kama tungeziiga. Ya kwanza ni ya National Economic Council ambayo kazi yake ni kumshauri rais wao kuhusu uchumi wa nchi yao na muelekeo wa uchumi wa dunia. Ofisi hii ni ya wachumi waliobobea.

Ya pili ni Congressional Budget Office ambayo kazi yao ni kupitia budget zinazowasilishwa, kuzipitia na kutoa maelezo ya namna zitakazo impact uchumi wa nchi. Ofisi hii ni uhuru ( non partisan) na watumishi wake wanaajiriwa kutokana na weledi wao katika taaluma yao na si kingine.

Serikali au Bunge wakitoa mapendekezo yeyote yenye ku impact uchumi wa nchi ( kupunguza au kuongeza kodi, kutoa huduma bure n.k.) ofisi hii inazipitia na kuelezea kuna mantik yeyote katika namna inavyopendekezwa zitalipiwa.

Kwa hapa kwetu, serikali ikisema itatoa huduma za bima ya afya kwa raia wote lazima tujue itagharamia vipi huduma hiyo. Serikali ikisema kuwa wanafunzi watasoma bure lazima waseme mishahara ya walimu na gharama nyingine zitalipiwa kutoka wapi.

Hii itatusaidia wote kujua uhalisia wa ahadi tunazopewa na serikali kujua athari ya mapendekezo yao kama ya kuongeza tozo kwa wananchi.

Amandla...
 
Taasisi hizo Tazania za nini,sisi Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi na Daktari wa Uchumi Mwigulu zinatosha kutoa mawazo ya kuchochea na kukuza Uchumi nchi.
Utaki hamia Burundi
 
Back
Top Bottom