Kuna kipindi nilikwenda show room moja kununua gari. Mwenye show room alikua hayupo wapo chawa. Nikauliza Bei ya gari, chawa kantajia Bei, nikamuuliza, je ikipoa? Kanijibu haishuki hata Mia. Nikamuambia chukua namba yangu Kati ya Leo na kesho Bei ikipoa nipigie hela iko mufuko ya shati. Chawa kakomaa, nikaenda zangu kijitonyama nikakuta gari Ile Ile Bei iko chini kwa milioni mbili halafu bado nikapozwa. Nikalipa fasta nikasubiri kesho yake nije kuchukua gari baada ya usajili.
Si ndio chawa kaanza kunitafuta na kuanza kushusha Bei. Nikamwambia I gave you 24 hrs. Time is up.
Nikawa napita Ile mitaa gari nikawa naiona haijapata mteja Hadi ikaanza kutu.