Mkuu,
Kama CCM wanatuma info zaidi kuliko vyama vingine (naongelea blogs) unatarajia nini? Wasiziweke simply kwakuwa wataonekana wanaipendelea CCM?
Let's be fair; vyama vya upinzani vinakalia habari sana, hata sielewi kwanini havitoi ushirikiano kwa blogs; wanataka wafuatwe ilhali CCM wanakuwa na waandishi wanaofuatilia na kutuma habari haraka kwa vyombo vyote vya habari.
Tarajia makubwa zaidi; CCM watalipia matangazo kwenye blogs, sasa wasiweke kwakuwa wapinzani watalalamika? Kwanini upinzani wasilipie japo kidogo? Hivi kweli hawana ruzuku ya kuweza kumudu kutangaza japo kwenye tovuti/blog nne au tano tu?