Kiranja Mkuu
JF-Expert Member
- Feb 18, 2010
- 4,219
- 4,608
Jirani aliibiwa simu miezi miwili nyuma nikiwa kazini, akasema wote waliokuwepo muda huo waende kwa mganga wa kienyeji mwenye Tv asilia ili wamuone mwizi wa simu. Huko walinyweshwa maji ya dawa yaliyochanganywa na damu mbichi. Tangu wakati huo afya yake imedorora sana, ameota vinyweleo vingi mwilini. Ana ndevu za sharafa na mustach, garden lavu pia limeshamiri kifuani. Kuweweseka hakumuishi usiku, raha hana. Je nimsaidiaje? Mimi ni mtafiti wa gas hivyo muda mwingi nakuwa site.
Kaka mmm!!!!!! hivi mpaka ukamluhusu mkeo aende kwa mganga wa kienyeji kwani yeye ndiye aliyeiba simu? Kama ww ni mtafiti wa gesi bila shaka umeenda shule. Na hilo lingekuwezesha kuachana na kasumba za ramli. Mwizi wa simu toka lini akaonekana kwenye luninga?? Kwa namna moja ama nyingine umechangia kwa mkeo kushiriki katika mambo hayo. Hata kama hakukuaga, ingekuwa unapinga hayo mambo pengine angeogopa kwenda huko. Sasa la maana hapa ni kumpeleka kanisani akaombewe na hayo mapepo/majini aliyopewa huko alikokwenda yamwishe. Na mwisho nakupa pole sana kwa yaliyokukuta. Mwizi huwa anatafutwa na Polisi, japo hawaaminiki siku hizi lakini ni bora kuliko mganga wa kienyeji.
Hao wengine waliokwenda na wao wanazo hizo "symptoms"?
Hizo "symptoms" ni za madawa ya vidonge ya kujichubuwa mwili uonekana mweupe, chunguza mkeo, kama anaanza kuwa muhindi, muarabu au mzungu ghafla, basi si ramli hiyo, ni hayo madawa ya kujichubuwa.
hao wengine hawana dalili zozote kama za mke wangu, ila mmoja alitoka mapunye mwili mziuma
Chukua GAS na Mbabuebabue mwilini.
Nywele zote zitafilia mbali. Ila fungua dirisha maana harufu ya nywele zinapoungua, mhhhhh.........
ushauri mwingine kama kuna sumu karibu unaweza ukanywa bila kupenda.
Khaa!
Pole sna kaka jaribu kumshitaki huyo aliempeleka mkeo kwa waganga!
Chukua GAS na Mbabuebabue mwilini.
Nywele zote zitafilia mbali. Ila fungua dirisha maana harufu ya nywele zinapoungua, mhhhhh.........
Kwani hii habari ni KWELI au ni mambo ya JF? Mie niliona kuwa jamaa anafurahisha JF na mie nikaona NIUNGE mstari......
Kama ni kweli basi nashauri waende kitengo cha kuchunguza Sumu mwilini.......
Au urudi kwa mganga huyohuyo na kumpa WARNING kuwa kama My Wife wako asipopona ndani ya wiki moja, basi utamshaki mahakamani ili aubebe msalaba wake kama Mkulo alivyoagiza............
Ushauri mwingine hauna tofauti na nguvu za giza!!!!!!!!!!!!!!!!
By the way nakushauri umpeleke mkeo hospitali fasta kabla hali haijawa mbaya zaidi.Maana inaonyesha kabisa kuwa moja ya athari za hiyo dawa aliyokunywa ni kuongezeka zaidi kwa homoni za kiume na ndio maana ameota vinyweleo miwli mzima.Hilo tatizo linatibika hivyo wahi mapema.