Kama nilivyosema mwanzo hilo si tatizo la huyo mganga, kuna makabila mengi yanakula/kunywa damu, tena mbichi na wanadunda. Sina haja hapa ya kumtetea mganga ila kwa hili la mganga "wajinga ndio waliwao".
Nipo hapa kusisitiza kuwa huyo dada anatumia mkorogo tena si wa kujipaka pekee, kaanza kukandamiza na vidonge na/au sindano. Hayo ndio maafa ya kutak weupe wa haraka na tusiokuwa nao.
Huyo mkeo analijuwa hilo na hilo la mganga ama anakudanganya ama kapatia sababu ya masahibu yaliyomkumba baada kupata dozi za mkorogo. Hakuna zaidi, ni hilo tu.