RIP Twaha Omar....Twaha Omar ninaye mfahamu mimi alikuwa mtu pole na mkarimu,akitokea kijiji cha kerenge nje kidogo ya mji wa Korogwe,ilimchukua muda mrefu kuonekana kipaja chake katika medani ya soka ukizingatia kabla hajajiunga na African Sport alihangaika sana kupata Timu ya uhakika,katikati ya miaka ya 80 alikuwa akichezea Timu moja ikiwa daraja la tatu Kilole United pale wilayani Korogwe alijaribu Biashara Shinyanga bila mafanikio.na baada African Sports kupanda daraja ndio na yeye alipopata nafasi kucheza ligi daraja la kwanza,na hawa African Sport walivutiwa na Twaha Omar walipomuona katika mchezo wa kirafiki kati ya Yanga v Nyota ya Korogwe..ingawa hakuwahi kuchezea nyota rasmi lakini mara nyingi hawa nyota katikati miaka ya 80 walikuwa na deturi ya kucheza mechi za kirafiki na timu kubwa zinapokuja mkoani Tanga hivyo kutokana na kipaji chake mara nyingi walikuwa wanamuomba ktk mechi kubwa za kirafiki...
Alipojiunga na African Sport kipaji chake kilionekana zaidi wakati ule akishirikiana ktk nafasi ya kiungo na marehemu Abasi Mchemba,Rafael John.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.Amin!