Twakimbiaje TARAWEHE ?

Twakimbiaje TARAWEHE ?

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
TWAKIMBIA TARAWEHE.


1)Ni Mara moja kwa mwaka,swala hii twaipata

Ingawa tunairuka,bila nafsi kutusuta

Nyumbani twa tawanyika,nini twaenda tafuta

Twakimbia tarawehe,kama tumeona nyoka.


2)Tunadai tumechoka,uvivu watukamata

Barakaze twaziruka,khasara tunaipata

Shahari ikitoweka,ndipo hapo tutajuta

Twakimbia tarawehe,kama tumeona nyoka.


3)Nyumbani tunapofika,mpira twenda tazama

Hili ni jipya gharika,imani zetu za zama

Kijana we chakarika,pepo inayo gharama

Twakimbia tarawehe,kama tumeona nyoka.


4)Imamu akigeuka,watu wapungua nyuma

Safu yazidi punguka,anakosa cha kusema

Salamu ikishatoka,wengine wanasimama

Twakimbia tarawehe,kama tumeona nyoka.


SHAIRI-TWAKIMBIA TARAWEHE

MTUNZI-Idd Ninga,Arusha

iddyallyninga@gmail.com

+255624010160.
 
Back
Top Bottom