Faith Luvanga
Member
- Aug 21, 2018
- 14
- 15
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha UPDP amesema kuwa Serikali yake itaandaa Muswada punde baada ya kuingia Bungeni kwa ajili ya unyanyasaji na udhalilishaji wa Wanawake ambapo Mahakama itatoa adhabu ya miaka 25 jela ili kutoa funzo kwa wengine.
"Tumejipanga vizuri, Serikali itatoa tuzo ya miaka 25 jela bila huruma kwa yeyote atakayejihusisha na udhalilishaji na unyanyasaji kwa mwanamke" Twalib Kadege
Ameongeza kuwa katika kumpa kipaumbele Mwanamke, Chama chake kilitoa uhuru kwa Wanawake na hawakuwabana. UPDD imewasimamisha Wanawake wengi katika kugombea nafasi za Ubunge na Ubunge wa Viti Maalum.
"Sisi tulitoa uhuru kwa Wanawake wote wanaoweza kugombea nafasi za Uongozi waje wajaze fomu, hatuweka vikwazo. Mfano kama Dar es salaam katika majimbo nane ambayo Chama chetu kimesimamisha wagombea nane (8) Wanawake ni saba na Mwanaume mmoja tu."Kadege
Kadege anasema katika nafasi za Ubunge wa Viti Maalum Wanawake walipewa nafasi na uhuru bila kuwekewa vikwazo katika kuchukua fomu za kugombea lakini pia Zanzibar Wanawake wengi wamegombea nafasi za Uwakilishi, Ubunge na Udiwani hivyo kufanya Chama chake kuwa na wagombea wengi wa nafasi za Uongozi.