TWAWEZA: Katika Watanzania watatu, Wawili wanataka Katiba Mpya

Ila sijaona chama Cha kumbukumbu Kama ccm mchakato wa katiba waliuanzisha wao wakausimamia wao walipoona ohooo hii katiba itatuchinja wenyewe wakalitelekeza jangwani.
Mkuu, mimi nakumbuka UKAWA ndio walikimbia bungeni wakiongozwa na msomi wa uchumi, prof. Lipumbu, tena ni baada ya kulamba posho zote za vikao.
 

Hii ni habari mbaya sana kwa group hii Jumbe Brown mama D na binamu zao.

Bila kumsahau Hangaya na wapambe wake.
 
ID za kulipwa hizi
 
Huu ukweli hawataukwepa hata wasemeje.
 
Watanzania wa wapi hao wenye elimu kubwa ya uraia....elimu hiyo ya KILIBERALI....watanzania wa wapi hao?!!!!!

Watupe SAMPLE SIZE ya research yao....watuambie waliwahoji watanzania wa KIWANGO GANI CHA ELIMU NA HALI GANI YA KIMAISHA....

Huku mitaani watanzania hao mnaojinasibu wala sijawahi kuwaona....kuwasikia.....hata huko VIJIJINI ni hivyohivyo........

SIEMPRE JMT
 
Wangesema wanaikubali Ccm ndio wangekuwa Elimu kubwa🤣🤣
 
Tafiti hupingwa kwa Tafiti mpya
 
Sema katika wanachadema watatu wawili wanataka katiba mpya. Watanzania wengi hawajui maana ya katiba.
 
Ripoti ya Warioba ilikuwa politically motivated...ilikuwa ni ya kisiasa zaidi ..ha...ikuwa ya kisayansi ile...ni Nani anataka katiba mpya...ni Nani anataka anataka eti serikali tatu?? Hovyo kabisa ile ripoti...Mimi nakuambia ukifanya utafiti wa dhati...watu wa Bara hawataki Muungano...Kama ni Muungano wanataka serikali moja na siyo ujinga wa serikali tatu
 

Low minds ndivyo wanavyofikiria. Ukimwuliza low mind nikupe nini, nikulipue ada ya chuo, ukasome au nikupe magunia ya udaga, atachagua udaga.

Hayo uliyoaandika ni uthibitisho kuwa uwezo wako wa tumbo umefifisha uwezo wa kichwa.
Elezea faida za katiba mpya hapa kwa mtanzania wa kawaida ambaye kila siku bado anahangaika kuweka chakula mezani. Low mind ni mtu asiyefafanua au kuelimisha jambo ila anategemea kutumia nguvu au lugha ya dharau kujaribu kunyamazishi wengine. Katiba zinasimamishwa au kubadilishwa wakati wowote ule hasa katika nchi zetu za Africa. Pesa kidogo tuliyonayo itumike -kupatia maji kwa kila mwananchi, afya bora , elimu kwa kila mtoto wa kitanzania , ajira kwa vijana na madawa hospitalini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…