MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Mengi yamesemwa, kwamba udukuzi ulitendeka kwenye upeperushaji wa matokeo baada ya uchaguzi, kwamba ushindi wa rais Uhuru sio halali na hii imepelekea hadi wana NASA kuomba nchi igawanywe mara mbili.
Sasa maswali ambayo sipati majibu yake, ni kwamba viongozi kwenye nyanja zingine zote hawakutegemea upeperushaji wa matokeo na ushindi wao ulihesabiwa mashinani na kutangazwa huko huko. Takwimu na tarakimu zinaonyesha chama cha Uhuru kilizoa viti vingi sana nchini, iweje wote hawa wapigiwe lakini waliowapigia kura wakose kumpa rais Uhuru.
Chama cha Jubilee kiliongoza kwenye idadi ya MCA ambao ni 582 wakati chama cha Odinga kikizoa 338
Uhuru ana wabunge 140 wakati Odinga akiambulia 61
Pia Uhuru anaongoza kwenye idadi ya magavana na maseneta, hii haingii akilini.
Japo inafahamika Uhuru alitumia nguvu nyingi ikiwemo raslimali za dola wakati wa kujinadi kwenye kampeni, lakini hili la ushindi ni wazi kwamba kashinda tena mchana, ni ukweli ambao mlengo wa upinzani unafaa kuukubali na kuupokea na kutafakari kipi kiliwakuta.
Leo hii hata kama mahakama ikiamua uchaguzi urudiwe, ifahamike hao viongozi wengi wa Jubilee waliochaguliwa watakua na nafasi muafaka ya kumfanyia kampeni Uhuru kwenye siku 60 ambazo zimeruhusiwa kikatiba. Ushindi wa pili utakua wa maamuzi makubwa ya kuhitimisha.
Mimi nafikiri upinzani ujitafakari, bado tunawahitaji lakini wajiangalie upya jinsi walinadi sera zao, ambazo mara nyingi zilikua za kutia madoa kwenye dola ilhali Uhuru alikita kwenye kueleza kile amekifanya kufikia sasa. Ni wazi Wakenya sote tunajua uongozi wa Uhuru ulikua na madoa doa ya matope, hivyo hatukuhitaji upinzani utumie hayo kama wimbo, wengi tulitegema kuambiwa nini kipo tayari kama mbadala wa utawala wa Uhuruto.
Rais Uhuru alikatiza na kupenya kwenye nchi yote kwa nguvu nyingi sana akijieleza. Kwanza alitumia uzinduzi wa reli ya SGR mpaka basi, yaani aliabiri treni na kuhutubia kila kituo alipokuta umati umemsubiri, ikumbukwe mamilioni ya Wakenya walikua wanafuatilia kwenye runinga zao. Upinzani ulijibu huo mtiti kwa kusema wazo la hiyo reli lilikua lao awali.