Twendeni shambani

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Huu msimu wa mvua; watu warudi mashambani wakalime.

Kumekuwa na utaratibu wa watu kulalamika vitu kupanda bei, hasa bidhaa za mazao.

Sasa kutokana na hizi mvua zinazoendelea kunyesha baadhi ya mikoa; zitumike kama fursa kwa kila mtu kwenda kulima angalau ekari tano (5) ili kupunguza kuwepo na upungufu wa chakula katika familia zao.

Nitashangaa sana, mtu yupo mjini, kulima hataki; halafu kipindi cha kiangazi anaanza kulalamika; mahindi, maharage, mchicha, alizeti n.k vimepanda bei; sasa unataka nani akakulimie?

Mimi kama mkulima, nitalima mazao yangu na kipindi cha kiangazi, nitakuuzia gunia la mahindi kwa shilingi laki mbili; hutaki, utakufa na njaa.

Msiseme sikuwaambia, weka tai chini ingia shambani; hakuna mkulima ambaye yuko tayari, ateseke sasa kwenye majaluba ya mpunga, halafu utegemee aje akuuzie mchele kwa shilingi 1000 kwa kilo.

Twendeni shambani; tusije kulalamika vitu vinapanda bei.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…