Twenzetu Kileleni miaka 63 ya Uhuru kuwafikia watu 200

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
Dsemba 5 mwaka huu kundi la watanzania 200 wakiongozwa na maofisa wa jeshi la wananchi Tanzania(JWTZ)litapanda mlima Kilimanjaro ilikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika.

Hili ni tukio la kipekee ambalo limekuwa kivutio kikubwa kwa watanzani wengi ambalo lilianzishwa rasmi mwaka 1985 na Generali Mrisho Sarakikya aliyepanda mlima huo kwa zaidi ya mara 40 kabla ya kukabidhi kijiti hicho kwa mkuu wa zamani wa majeshi ,Mwita Waitara.

Jenerali Mrisho Sarakikya ni miongoni wa watu maarufu hapa nchini kwa mchango wake katika maeneo mbali mbali hasa katika huduma za kijeshi .

Kupanda kwake mlima kilimanjaro ilikuwa ni sehemu ya maandalizi yake ya kuwaongoza wanajeshi wa Tanzania kwenye shughuli mbalimbali na mwaka 1994 ndipo alipokabidhi kijiti hicho kwa Waitara.

Mwaka 2006 alikuwa miongoni mwa watanzania wachache waliopanda mlima Kilimanjaro akiwa na umri mkubwa wakati huo akiwa na umri wa miaka 61 aliamua kupanda mlima huo kama sehemu ya kuhamasisha watu kupanda mlima huo kama sehemu ya kuhamasisha kuhusu umhimu wa afya na ustawi wa mwili..

PIa zoezi hilo ilikuwa ni kuieleza jamii kuwa umri siyo kikwazo cha kufikia malengo makubwa .

Jenerali Sarakikya ambaye ni mkuu wa majeshi mstaafu, kupanda kwake mlima kilimanjaro ilikuwa ni njia ya kuonyesha uzalendo,nguvu,umoja pamoja na kuonyesha mfano wa ujasiri na ari kwa jamii yake na kwa vijana wengi.

Akizungumza na waandhishi wa habari hivi karibuni katika uzinduzi wa kampeni hiyo,mkurugenzi wa kampuni ya wakala wa Utalii nchini ya Zara Tours,Zainab Ansell maarufu kama mama Zara,alisema huu ni msimu wao wa nne katika kuhamasisha kampeni ya watanzania kupanda mlima huo na safari hii wapanda mlima 200 wanatarajia kupandas mlima huo kupitia lango la Marangu.

Amesema tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan azindue Filamu ya Royal Tours katika mkakati wa kutangaza vivutio vya utalii nchini,milango imefunguka na kumekuwepo na ongezeko kubwa la watalii kila mwaka .

Mwanahabari na mtangazaji nguli wa zamani wa Shirika la Utangazaji na BBC la Uingereza,Salim Kikeke ambaye amekuwa mhamasishaji mkubwa wa kampeni ya Twenzetu Kileleni,amesema kwa sasa kuna hamasa kubwa ya watanzania wengi kupenda kupanda mlima Kilimanjaro.

Anasema mwaka 2021 alipopanda mlima huo kwa mara ya kwanza na kurusha matangazo ya Moja kwa moja kupitia BBC World News akiwa kilele cha Kibo,kulikuwa na namba ndogo ya watalii ikilinganisha na sasa ambako kuna uongezeo kubwa la watalii .

Kikeke akatoa wito kwa watanzania kujenga utamaduni wa kupanda mlima Kilimanjaro ikiwa na lengo kuhamasisha utalii wa ndani na kurejea tukio la kigaidi mwaka 2010 ambako Kenya ilishambuliwa na kikundi cha kigaidi ya Al-Shaabab ambako sekta ya utalii iliyumba baada ya wageni wengi kufuta safari zao za kuitembelea Kenya.
Anasema Kenya iliimarisha kampeni ya kuhamasisha utalii wa ndani na kuongeza namba kubwa ya wakenya kutembelea vivutio vya utalii.

Pia alipongeza hatua ya serikali kwa kushirikisha sekta binafsi katika kampeni ya kuhamasisha watanzania kupenda kutembelea vivutio vya utalii akiangazia Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(Tanapa) na Bodi ya Utalii nchini (TTB) kwa kuonyesha njia.

Akamtaja Rais Samia Suluhu Hassan Kama kiongozi (Guide)namba moja kaktika kampeni ya kuhamasisha watanzania kutembelea vivutio vya utalii haSa baada ya kuzindua filamu hiyo ya Royal Tour.

TUKUTANE DESEMBA 5 MARANGU GATE
 
Attachments

  • Zara 1.jpg
    Zara 1.jpg
    687.9 KB · Views: 2
  • Zara 2.jpg
    Zara 2.jpg
    582.4 KB · Views: 2
  • Zara 3.jpg
    Zara 3.jpg
    613.2 KB · Views: 1
  • uhamiaji.jpg
    uhamiaji.jpg
    675.8 KB · Views: 2
Ning

Vigezo na msharti miongoni mw ao watu 200 wanaopanda ikiwezekana niwe mmoja wao
 
Back
Top Bottom