GJ Mwanakatwe
JF-Expert Member
- Mar 26, 2011
- 241
- 27
Kuna taarifa kwamba twiga wanne walisafirishwa kinyemela kupitia uwanja wa ndege wa KIA wiki mbili zilizopita kwenda ughaibuni.Hizi habari zinashangaza sana,yaani twiga walivyowakubwa wapitishwe KIA bila kuonekana na vyombo vya usalama uwanjani hapo? haiwezekani hata kidogo. Hii inaonekana kuna mtandao mrefu wa wizi wa maliasili za nchi, na huu ni ufisadi mbaya kuliko mingine kwa kuwa wanyama hao na wengine watakwisha halafu tutakosa mapato, ni afadhali waibe fedha tutapata fedha nyingine kuliko kuiba wanyama wetu, maana sasa itakuwa wanatuibia mtaji.Ni muhimu suala hili lifuatiliwe kwa karibu na wote walihusika wachukuliwe hatua kali za kisheria.