TWIRWANEHO yatangaza kujiunga rasmi na AFC/M23

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
350
Reaction score
576
Kundi la wapiganaji TWIRWANEHO, huko Kivu kusini, limetangaza rasimi kujiunga na kundi la AFFC/M23.

Baada ya kifo cha aliekuwa kiongozi wa kundi hilo, General Michael RUKUNDA, AKA MAKANIKA, kwa shambulio la ndege isiyo na rubani ya serikali, lililoondoa uhai wake, uongozi wa kundi hilo kwa sasa anao Brigedia General Charles SEMATAMA.

Sematama, ametangaza haya, baada ya kifo cha kiongozi mwenzake. Amesema, awali, kundi hilo lilikuwa likihakikisha linakabiliana na uvamizi wa jeshi la serikali, na vikundi vya kigaidi kama mai mai na FDLR, na kwamba wao hawakuwahi kulishambulia jeshi. Lakini kwa sasa, baada ya AFC/M23 kufika maeneo ya makazi ya wanyamurenge(MINEMBWE), wamejiunga rasmi na kundi hilo kwa lengo la kuongeza nguvu, kuhakikisha serikali inawajisbishwa.
 
Sijakuelewa!!
M23 na uchafu wote unaendelea huko congo unakusaidia Nini kuondokana na hali ya umaskini, kwa kuanzia na ww na jamii inayokuzunguka??....kama hujaelewa na hapo waambie mods wachukue zile spika mpya alizo nunua founder wa jf, uwekewe maskioni ili sikio lizibuke uskie vizuri, sawa dogo??
 
Hujavuta bangi kweli wewe?
 
Kwahiyo hivi vikundi vya Waasi vikiungana si itakuwa ni balaa dhidi ya Serikali ya Etienne Tshisekedi?!
 
Sawa babu. Sasa, povu la nini? FARDC na FDRL yenu uliona ndo msaada kwako sasa! Pole! Hakuna makuu yasiyo na ncha.
 
Kwahiyo hivi vikundi vya Waasi vikiungana si itakuwa ni balaa dhidi ya Serikali ya Etienne Tshisekedi?!
Pale hakuna serikali tena bro. Kila mmoja ameshamuachia apambane na hali yake.

South Africa yenye kihelehele, pale inangojewa na Israel. Round ya kwanza, kapigwa knock out, hajaacha. Ngoja waingie mzigoni sasa
 
Nasikia Vikosi vya Sauzi vimekaribia Kalemie.
 
Kundi la wapiganaji TWIRWANEHO, huko Kivu kusini, limetangaza rasimi kujiunga na kundi la AFFC/M23.

Baada ya kifo cha aliekuwa kiongozi wa kundi hilo, General Michael RUKUNDA, AKA MAKANIKA, kwa shambulio la ndege isiyo na rubani ya serikali, lililoondoa uhai wake, uongozi wa kundi hilo kwa sasa anao Brigedia General Charles SEMATAMA.

Sematama, ametangaza haya, baada ya kifo cha kiongozi mwenzake. Amesema, awali, kundi hilo lilikuwa likihakikisha linakabiliana na uvamizi wa jeshi la serikali, na vikundi vya kigaidi kama mai mai na FDLR, na kwamba wao hawakuwahi kulishambulia jeshi. Lakini kwa sasa, baada ya AFC/M23 kufika maeneo ya makazi ya wanyamurenge(MINEMBWE), wamejiunga rasmi na kundi hilo kwa lengo la kuongeza nguvu, kuhakikisha serikali inawajisbishwa.
DRC kupata uhuru soon
 
Nasikia Vikosi vya Sauzi vimekaribia Kalemie.
Hahahahahahaha unasikia tu. Vitu bado vipo Lubumbashi, vingine vimekwama Bujumbura. Kalemie vitaendaje mkuu! Ziwa lipo under control ya M23, barabara ndo hivo!!!!
 
M23 na uchafu wote unaendelea huko congo unakusaidia Nini kuondokana na hali ya umaskini, kwa kuanzia na ww na jamii inayokuzunguka??....kama hujaelewa na hapo waambie mods wachukue zile spika mpya alizo nunua founder wa jf, uwekewe maskioni ili sikio lizibuke uskie vizuri, sawa dogo??
Mkuu antibiotic unaumwa?
 
Back
Top Bottom