BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Inaonekana ni ngumu sana kwa hii mitandao kuwa na idea za utofauti ambazo hazifanani na platform nyingine; sijui ni uzembe wa kubuni idea mpya au idea mpya zimeisha.
Twitter imetangaza mabadiliko mawili ambayo yanafanana kabisa na TikTok na Instagram Reels.
1️⃣ Twitter inaweka sehemu ya “Video for you” ambayo itakuwa kama Instagram Reels. Sehemu hii itakuwa inaonyesha video ambazo utazipenda; na algorithm itakuwa inaziweka kuendana na interests zako.
2️⃣ Kingine, video zitakuwa katika mfumo wa Full-Screen kama video za TikTok. Ukitaka kuitazama video na kuifungua inachukua style ya full screen na chini itakaa caption na sehemu za likes, retweet na comments.
Mabadiliko haya yameanza kwa baadhi ya watumiaji wa iOS na Android. Itabadilika kwa watumiaji wote.
Credit: Apollo ( Instagram)