Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Baada ya kusubiri kwa muda mrefu, hatimaye mtandao wa kijamii wa Twitter umetangaza kuacha kukata picha na sasa hautalazimika kufungua kuona picha kwa ukubwa kamili.
Mtandao huo ulitangaza miezi kadhaa iliyopita kuwa unajaribu mwonekano huo mpya, kabla ya kuanza kutumika rasmi. Twitter ilikuwa ikikata picha zote zisizokuwa na uwiano wa 16:9, hali iliyokulazimu kufungua picha ili kuiona kwa ukubwa kamili.
Mtandao huo ulikuwa ukilalamikiwa kwa kutokuwa na usawa katika kukata picha, baadhi ya watu wakilaumu kuwa mfumo wa kukata picha (algorithm) ulikuwa ukiwapendelea wazungu kuliko watu wenye rangi nyeusi.
Lakini baada ya sasisho hili, utaweza kuona picha kwa ukubwa kamili bila kulazimika kuifungua kwanza.
Baadhi ya watumiaji hawakusita kuonesha furaha yao kwa kuchapisha picha “ndefu” ambazo awali zisingeweza kuonekana kwa ukubwa kamili.