Nimejaribu kupiga hesabu ndogo, ukikamata vinyonga kumi tu na ukafika nao dsm kutoka hapo Morogoro una wastani wa Tsh 1,00,000/ safi, kumbuka mtaji wako hapa ni muda wako,nauli na posho ya vijana,ukiweza kumpata jamaa wa maliasiri akakwambia vinyonga walipo na posho yake ( Vibali kama kawaida)vijana wa kijijini ukimpa laki moja akukamatie vinyonga, baada ya sekunde chache una vinyonga lundo. Mchana huo huo unageuza na Abood Bus hadi kwa mteja wako na biashara imeisha.
Ukisoma vizuri lile gazeti,unagundua kwamba,wale jamaa wa maliasiri wanajua vizuri soko la hawa vinyonga na dealers ni kina nani.