Baba_Enock
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 7,076
- 2,457
Mkuu halafu cha ajabu hao makamanda wenyewe ni wazee wazima kama yule wa mchafukoge sijui jibaba kabsaa
wakuu,
mara kwa mara nimekuwa nikisikia kwenye vyombo vya habari kuwa mtu fulani amesimikwa kuwa kamanda wa ccm. Na siku za hivi karibuni kuna amesimikwa kamanda wa uvccm kibaha.
ningependa kufahamishwa hiki cheo cha u-kamanda, ni nini hasa nafasi/madhumuni/malengo yake katika chama cha mapinduzi?
be
Mkuu halafu cha ajabu hao makamanda wenyewe ni wazee wazima kama yule wa mchafukoge sijui jibaba kabsaa
Ukamanda ni njia rahisi ya kuonesha kuwa unakubalika na vijana na ukiwa tayari kugombea basi tayari una kaujiko. Utaona makamanda wengi leo hii ni wale ambao wanatarajia hata kugombea majimbo ambayo wao tayari ni makamanda!
Kazi yao kubwa ni kuchekesha. in ashangaza kwa chama kikongwe kama hicho na kinachodai kuwa serious kinakuwa na mambo ya ajabu na ya kipuuzi kabiksa kama haya. Ndiyo maana nchi imekwama.
Kama una haja ya kuona cartoon ya bure, ngoja siku CCM wanafanya Mkutano wao Mkuu (general Congress) kule Kizota Dodoma. Hawa makamanda kutoka nchi nzima huwekwa pamoja wakiwa wamevaa 'sare' zao. Nimeweka mabano bcoz siyo sare per se kwani kila moja ina mshono wa peke yake na huunganishwa kwa ile rangi tu ya green, ambayo nayo hutofautiana.
Kutokana na umri wa wengi wao, huwezi kuacha kuvunja mbavu jinsi wanavyoonekana -- ni vikaragosi vimekwisha kazi! na ngojea basi wanapoimba. Akina Tom na Jerry ni wanafunzi tu kwa kuvunjisha watu mbavu.