Uaandaaji wa Barua kwa ajili ya Ufadhili (Appeal Letter)

Joined
Feb 5, 2022
Posts
38
Reaction score
60


"Appeal Letters" ni barua ambayo huandaliwa na Taasisi kwenda kwa mfadhili (supporter) kwa ajili ya uombaji wa ufadhili. Barua hii, ni nyenzo muhimu ya mawasiliano baina ya Taasisi na Mfadhili. Unapoandaa barua hii, hakikisha unaanza kwa kueleza historia ya Taasisi yako. Vitu vingine muhimu ambavyo vinapaswa kujumuishwa kwenye barua hii ni kama ifuatavyo;
  • Maelezo juu ya mradi au tukio linalohitaji ufadhili. Hii ndio sababu kubwa ya kuandika barua hii, hivyo basi unapaswa kueleza "a good story" juu ya mradi au tukio lako, stori yako lazima ijikite kwenye kuonyesha kwanini ni muhimu mradi au tukio kufanyika, pia kuna umuhimu gani wa mfadhili kuwa miongoni mwa wafanikishaji wa tukio/mradi huo. Na hapa si lazima iwe mradi au tukio pekee, hata ufadhili wa shughuli za kila siku za Taasisi.
  • Maelezo juu ya Taasisi (Hook) Eleza kwa namna gani Taasisi yako imekuwa ikileta mabadiliko chanya katika jamii kupitia programu na miradi yake, hii ndio sehemu ya kumvuta mfadhili. Mfano kama Taasisi yako inajikita na Mradi wa kukusanya ngua/vifaa mbalimbali na kuwapatia watoto yatima, ni vizuri kuonyesha picha za watoto hao kabla na baada ya kunufaika na mradi wa Taasisi yako.
  • Hitajio lako la ufadhili/fedha. Hapa eleza kiasi cha fedha unachohitaji (ikiwa unahitaji fedha), pia uonyeshe ni kwa namna gani fedha utakazopata zitaweza kuleta mabadiliko. Kwa mfano; unahitaji fedha kwa ajili ya mradi wa kununua vifaa vya shuleni kwa ajili ya watoto yatima, onyesha kwa mfano Tsh 300,000 itanunua mabegi 30, Tsh 200,000 itanunua daftari 50 n.k
  • Uwiano ulipo baina ya dhima au utume wa Taasisi yako (mission) na Mradi au Tukio unalotaka kufanya. Lengo la sehemu hii ni kumuonyesha mfadhili kwamba wazo la Mradi au Tukio halijaibuka ibuka bali lipo katika mipango na malengo ya Taasisi.
  • Ombi la ufadhili. Hii ni sehemu ya mwisho ya barua. Hapa unapaswa kuomba ufadhili wa pesa, vifaa au watu wa kujitolea kwa ajili ya utekelezaji wa mradi au tukio lako. Namna nzuri ya kuomba ni kumueleza mkusudiwa ni nini anaweza kufanya ili kufanikisha Mradi au Tukio. Ikiwa mfadhili unaemuomba alishakufadhili kiasi cha fedha hapo awali, taja kiasi alichotoa hapo awali na muombe aongeze kiasi fulani (zingatia; udogo wa kiasi) sio kwamba hapo awali alikufadhili Tsh 500,000 na sasa unamtaka aongeze Tsh 3,000,000, usifanye hivyo.


OMAR MSONGA (BA. PPM &CD)
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…