Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Kumekuwa na mashindano ya kuongelea uadilifu Tanzania mwaka huu na hasa kuangalia wagombea Urais.
Kuna kundi moja kwa nguvu linadai Mgombea Edward Lowassa ni fisadi mkubwa na hastahili kuwa Rais kwa kasha ya Richmond na tuhuma nyingine ambazo hazitajwi bali zinatishiwa kutajwa. Aidha inatajwa "laana" ya Baba wa Taifa mwaka 1995 kuwa kigezo cha kumtuhumu uchafu.
Ama kuna kundi lingine linasema Mgombea Magufuli ni fisadi wa kuuza nyumba za Serikali na kujinufaisha mwenyewe, wanaangalia ufisadi wa wizara yake na suala la Samaki wa Magufuli.
Zote hizi ni tuhuma ambazo pamoja na kuweko kwake, wote Lowassa na Magufuli waliaminiwa na Rais, Serikali (Bunge) na hata chama Tawala kuendelea na madaraka na vyeo mbali mbali ndani ya serikali.
Taifa limekuwa likirushiana vijembe vya ufisadi, viongozi waandamizi wa Serikali wamekuwa wakitishiana na kutoa kauli za kurubuni (blackmail) kuwa wana mengine mengi ya kusema lakini wanasubiri wachokozwe zaidi au watuhumiwa wabishe.
Najiuliza, ikiwa Katiba ya nchi inatamka bayana wajibu wa kulinda nchi kutokana na uhujumu wa aina yeyote, iweje leo kuwe na wananchi na hata watendaji ambao wanasema wakisema yale yote na kufungulia bomba, nchi itaangamia. Je wanaitendea nchi haki kwa kutunyima uhondo wa "udaku" hukku ni wajibu wao kikatiba kusema kweli na kuliondola Taifa mzigo wa laana ya Taifa linalopenda Rushwa, Ufisadi na Takrima?
Mfano, kuna mambo mawili makubwa sana nchini kwetu ambayo yalizimwa kimya kimya na tukaambiwa haya yatatishia usalama wa Taifa hata kuweza kuingusha Serikali: Suala la Meremeta na Richmond.
Ni siri gani kuu katika tuhuma na Ufisadi wa Meremeta na Richmond ambao ni mkubwa sana kuwa tutoe kafara utu na uadilifu kwa kunusuru Serikali ambayo bila haya kutokana na maamuzi na utendaji dhaifu, nchi imeingia hasara?
Ikiwa Meremeta ilitugharimu (fedha zilizotolewa taarifa, bado mengine mengi yanafichwa) si chini ya dola za kimarekani Milioni 200, kulipia "deni", kati ya mwaka 1996-2006, je fedha hizo zingeweza kujenga hospitali ngapi za viwango kubalika kwa kila wilaya Tanzania (zingatia umahiri na uimara wa shilingi miakak hiyo)?
Je mradi wa Richmond, pamoja na kutoa kafara nusu ya Serikali kwa waziri mkuu kulazimika kuwajibika, lakini mkataba ukaendelea na mpaka leo umerithishwa mtu wa tatu, lakini bado kuna utata wa ukweli wa jambo la Richmond, je fedha za mkataba wa Richmond zingepewa Tanesco ijinunulie mitambo yake yenyewe ya ziada au tungefuta gharama za muda mrefu za mkataba wa Richmond (capacity charges) kwa kuuvnja mkataba, fedha ambazo tungeokoa zingeweza kujenga vyuo vya ufundi au kujenga vito imara vya polisi.
Ni wzi kabisa kuwa kama taifa tumeuzoea mfumo wa ufisadi, rushwa na takrima na leo tunachagua ni ufisadi upi unafaa tunyamazie na ufisadi gani tuupigie kelele.
Kwangu mimi, ufisadi hakuna ufisadi mkubwa au ufisadi mdogo. Mwizi wa kuku na mwizi wa gari wote ni wezi. Fisadi wa Richmond, fisadi wa Meremeta, fisadi wa Kiwira, Fisadi wa mikataba ya madini na fisadi wa kuuzwa nyumba za serikali wote ni mafisadi. Hakuna aliyebora au aliye na unafuu.
Ufisadi ni sawa na uzinzi. Ni kukiuka maadili na kiapo, tunasifia sana kuchepuka kwa watu nje ya ndoa, Ufisadi hauna tofauti na kuchepuka kwenye ndoa maana kote kunavunja maadili na viapo.
Sasa ukiangalia ripoti ya Warioba ya mwaka 1996 kuhusu masuala ya Rushwa, kero zote tunazozitaja leo na kuzipigia kelele, ziliorodheshwa mwaka 1996.
Swali ni hili:
Kwa nini Serikali ya Mkapa na Kikwete hazikulipa tatizo hili kipaumbele na udharura kutatua tatizo hili sugi ambalo limemea katika jamii nzima na kuomba au kutoa chai sasa ni wajibu usio na woga wala noma?
Je Bunge, vyama vya siasa kwa nini pamoja na kujulikana kuwepo kwa mchanganuo huu ambao uligharimu Taifa kodi s=zetu, lakini faili likawekwa kabatini kupata utando na mavumbi, vilikaa kimya bila kuishinikiza Serikali Kuu kufanyia kazi?
Leo hii, wagombea wa Urais Magufuli na Lowassa ambao wote ni watuhumiwa wa Ufisadi, wanadai kuwa wakiingia Ikulu watalishughulikia tatizo la rushwa na ufisadi.
Sisi kama jamii, tunashindana kupigana vijembe vya nani fisadi zaidi na nani heri awe Rais.
Hata wanaogombea ubunge na udiwani kuna sehemu kubwa sana ya watu wenye tuhuma za ufisadi, ujangili na hata uuzaji wa madawa ya kulevya na ujambazi. Lakini akiwa ni mgombea wa chama chetu, tutamsafisha na kusema huyu anaaminika zaidi.
Ripoti ya Warioba inaonyesha mengi makubwa sana ya mfumo wa rushwa na ufisadi.
Nikitafakari kwa kina mchakato wa vyama vya siasa kutafuta wagombea hata kutangaza wagombea, rushwa na ufisadi umetawala na hata kejeli imetumika kudhalilisha maana ya Uadilifu pale vyama vya CCM na ushirika wa Ukawa walipokiuka katiba, kanuni na misingi ya kidemokrasia ndani ya katiba zao na kutuletea wagombea hawa wawili wa Urais; JOhn Magufuli na Edward Lowassa.
HIvyo basi kwa kuwa najisi imefanyika katika suala la uadilifu kwa uchaguzu huu wa 2015, hakuna mtu au kundi lenye haki kudai uadilifu au Utakatifu.
Kama wananchi tumchague tumpendaye kwa utashi lakini si kwa unafiki wa kudai huyu ni mwadilifu zaidi kidogo kuliko mwingine au kudai huyu ni fisadi kidogo kuliko fisadi mkubwa.
Tunachopaswa kufanya kwa kina ni kulazimisha matokeo na kuunswa kwa Serikali ambayo itaifanyia kazi Ripoti ya Warioba kwa dhati na kwa udharura, baada ya kuapishwa.
Tuunde tume ya kulipitia suala la Ufisadi sawa na lile la Desmond Tutu kule Afrika Kusini, ili tulitatue tatizo hili kwa amani bila upendeleo wala dhihaka kwa mfumo wetu wa sheria.
Jisomeeni sehemu ya ripoti ya Warioba inayoongelea sisi wananchi na rushwa ndogondogo na watendaji na rushwa kubwa kubwa.
http://www.amielandmelburn.org.uk/collections/soundings/07_198.pdf