Ni kweli Yen imekuwa na nguvu sana dhidi ya USD kwa sasa na hii imesababisha export yao kushuka maana vitu vya Japan vimekuwa ghali zaidi na inasemekana hii ni mojawapo ya sababu za kuenguliwa kwenye nafasi ya pili ya nchi yenye uchumi mkubwa duniani na China. China wao wamefix pesa yao kuwa chini ili waweze ku-export zaidi ndo maana pamoja na wafanyabishara wengi sana wakiwemo wa-Tanzania kununu sana vitu China ila cha ajabu hakuna bureau de change hata moja TZ inayouza Yuan ya China.
Mahali pengine unapoweza kupata gari kwa bei rahisi ni Uingereza japo Paundi nayo imekwea juu lakini bei zao bado ziko chini. Tatizo kubwa, wauzaji wa Uingereza hawana mitandao mingi yenye kuonyesha magari na bei zake kama ilivyo kwa Japani. Wao mpaka uwe na mtu unayemfahamu huko ili akusaidie kuulizia kwa wauzaji. Nina rafiki zangu wawili wamenunua huko kwa bei nafuu zaidi kuliko Japan.