Ualimu ni taaluma mama inayohusika moja kwa moja na kujenga taifa lakini inasulubiwa. Hali hii itaisha lini?

Ualimu ni taaluma mama inayohusika moja kwa moja na kujenga taifa lakini inasulubiwa. Hali hii itaisha lini?

MWALIMU DAIMA

Senior Member
Joined
Mar 4, 2023
Posts
129
Reaction score
263
Habari Wana JF

Hope wote ni wazima, kwa upande wangu Mimi ni mzima wa afya. Niende moja kwa moja kwenye mada, kwa miaka mingi sasa taaluma ya ualimu imekuwa ikichukuliwa kama taaluma dhaifu, taaluma hii imedharaurika kwa muda mrefu.

Maisha ya walimu ni duni sana, maslah ya walimu bado yapo chini, mazingira ya kazi pia bado sio rafiki, ukilinganisha na taaluma nyingine.

Swali ambalo najiuliza daima inakuwaje taaluma hii mama ambayo inahusika moja kwa moja na kujenga taifa Ina sulubishwa?

Cha ajabu Zaidi chama Cha walimu pia kina lalamikiwa na walimu Wengi kuwa hakitetei haki na maslah ya walimu hii ni aibu na hatari sana. Walimu wanafanya kazi wakiwa na vinyongo na chuki moyoni mwao , Hali hii itaisha lini?

Walimu tumekuwa wajinga kiasi hiki cha kushidwa kusimama kwa pamoja na kupinga ukandamizaji huu,
Walimu tumekuwa waoga huku maslah yetu yako finywa, HAPANA ni Wakati sasa walimu kuamka na kupambana kwa ajiri ya haki na mustabali wa taaluma yetu.

# teacher movement
 
Kama mimi nimemaliza 2020 waliifuta diploma ya ualimu tukaishia kutokua na muelekeo natamani ifike mahali hata wanaoisomea wawe wanathaminiwa walimu mpaka wanaamua kufanya biashara zingine ili waweze kujikimu kwenye maisha
 
Hali itaisha siku ccm itakapotoka madarakani. Hiki chama ndiyo chanzo cha matatizo yote yanayo wakumba Watanzania.
 
Tumechoka bana poor mind people discuss people!!!
 
Hali hii itaisha mpaka pale atakapokuja kiongozi atakayekuja kuthamini waalimu, watu maalum wa vyombo vya ulinzi na usalama, na madaktari.

Ni watu muhimu sana! Sana! Sana! Kwenye taifa lolote lile duniani.
 
Back
Top Bottom