SoC02 Ualimu si wito, ni taaluma yenye sifa na tija kwa taifa la Tanzania, tukiwathamini Walimu tumeithaminisha Tanzania

SoC02 Ualimu si wito, ni taaluma yenye sifa na tija kwa taifa la Tanzania, tukiwathamini Walimu tumeithaminisha Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Yombo08

Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
20
Reaction score
10
UALIMU SI WITO, NI TAALUMA YENYE SIFA NA TIJA KWA TAIFA LA TANZANIA, TUKIWATHAMINI WAALIMU TUMEITHAMINISHA TANZANIA.


HALI YA WALIMU HIVI SASA? NI FUMBO LISILO NA MAJIBU

Kama Taifa tulipofikia hapa sasa tume muacha Mwalimu na maswali mengi hata pengine ambayo hakusitahili kujiulza, na mengine hawezi hata kuyapatia ufumbuzi. Tumewaacha watanzania midomo wazi, wakipigwa na mshangao hawaelewi ualimu ni taaluma au ni kazi kama kazi nyingine isiyoheshimika, Wadau wa elimu na watanzania wamekuwa na maswali mengi. Je? Ualimu ni sifa au cheo? Alipewa na kina nani? Na kwa kazi gani? Na je? Anathaminika? Kazi yake inaendana na mshahara anaopata? Mazingira anayo fanyia kazi ni rafiki au ndio basi liende? Jamii inamchukulia ni mtu wa aina gani? Je? Kutoka na haya yanayoendelea kuna watu wenye mapenzi kutoka moyoni ya kuja kuwa waalimu kama ilivyokuwa zamani? Ukimaliza hayo ongezea na haya Je? Ni kweli kuna mwalimu mzalendo kwa taifa letu la Tanzania siku hizi tofauti na kipindi cha nyuma? Na Vipi kuhusu hali za watoto wetu wakike na kiume huko shuleni kama walimu wao kutwa kuchwa wanalia na kulalamika?

Haya ni baadhi ya maswali machache ambayo Wadau wa elimu hujiuliza, juu ya hatima ya walimu inchini Tanzania. Na maswali haya hayajapatiwa ufunbuzi kila uchwao, bali yakifika sehemu husika hupigwa dana dana kama Lionel Messi na Christiano Ronaldo. Ahadi za kutatua changamoto za walimu ni nyingi kuliko hata changamoto zenyewe, lakini ni ngapi Zimetimizwa au japo kuonyesha jitihada za kushughulikia changamoto hizi.

NANI WA KULAUMIWA?
Kwa jinsi hali ilivyo sasa, Wadau wa elimu na watanzania kwa ujumla wanashindwa kung’amua nani wa kulaumiwa katika hili Je, ni serikali kwa kushidwa kuwahudumia waalimu na kutatua changamoto zao Au waalimu wenyewe kwa kushindwa kusimama na kutetea hoja zao za Msingi. Ukirudi nyuma unaona waalimu wamepambana sana katika kutaka haki zao na ilifika hatua hata wakaanzisha Mgomo 30, July Mwaka 2012. Ambao ulikua ni Tanzania nzima. Waligoma kufanya kazi mpaka shida zao zitakapotatuliwa, na Mgomo huu ulikuwa ukipewa nguvu na zaidi ya asilimi 97.5% ya waliwmu wote Tanzania ( Christian Bwaya, 2012)

Screenshot_20220811-150613.png

Pichani ni walimu Mkoani Tunduma wakiwa wamefunga njia ya kuelekea boda la tunduma, Mwaka 2012 (Chanzo, Jamii forums, 2012, habari na hoja mchanganyiko).

Pia kulikuwa na Mgomo Wa chini kwa chini wa waalimu Mwaka 2017 wakiwa na Kauli mbiu ya (TAYE) “Teach as you earn” Yaani fundisha kulingana na kipato chako. ( Jamii forums, “Habari na hoja mchanganyiko” March 1, Mwaka 2017) Wakiwa kinyume na mshahara wanaopata na makato ya (PAYE) “Pay as you earn” Yaani lipa kulingana na kipato chako.


NINI KIFANYIKE?
Imefikia hatua watu wanasema ualimu ni wito, sasa hauchukuliwi tena kama taaluma au fani ambayo inaweza kumpatia mtu heshima, kumpatia riziki ya kila siku na kulijenga taifa. Misingi mibovu na mitazamo hasi iliyotengenezwa juu ya walimu inalihalibu taifa la kesho, kwani Mwalimu ndiye anaye litengeneza na kulipika taifa la kesho, kumbuka kama mpishi akiwa na utungu (hasira) hakika atakachokitengeneza hakitakuwa bora bali kitaidhihirisha hasira yake. Hivyo basi kama taifa, wadau, serikali na sekita binafsi, tuna takiwa kubadilisha hili na mitazamo ya watu, ili kuirejesha heshima ya taaluma ya ualimu iliyopotea katika kipindi hiki cha sasa kwa ajili ya faida ya Tanzania yetu ya kesho, kupitia mkuzaji wetu wa sasa ambaye ni mwalimu.

Yafuatayo ni mapendekezo kwa Serikali, wadau wa elimu na sekita binafsi kwa ujumla, katika nyaja tofauti tofauti.


Moja, (CWT) Chama cha Walimu Tanzania.

Kuimarishwa kwa (CWT) Chama cha Walimu Tanzania, Sote tunafahamu ya kuwa chama hiki kinafanya kazi katika kutatua changamoto na shida zinazowakabili waalimu lakini sio kwa kiwango cha kuridhisha au kinacho hitajika. Nguvu ya ziada inahitajika ili kuzidisha ufanisi wa chama hiki.

kwanza kabisa ni kuongezwa kwa ofisi au matawi ya chama kwenye vijiji na maeneo ambayo ofisi za chama hiki hazijawekwa ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa walimu wa maeneo ya vijijini pia

Jambo lingine, ni kutumia teknolojia au mfumo wa internet katika kuwaunganisha walimu wote Tanzania, eidha kwa kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook, Whatsapp, Telegram, Instagram na Twitter au kutumia blogs kama njia ya kuwaleta walimu pamoja na kuwapa nafasi ya kutoa hoja zao.

Makongomano na washa mbalimbali zinazowaleta walimu pamoja katika kujadili changamoto na maswala mbalimbali yanayowakabili ziongezwe kwa wingi, kwani washa hizi na makongamano hutoa fursa kwa walimu kueleza hali halisi wanayokutana nayo mashuleni ambayo hata viongozi wa CWT hawayafahamu.

Pili, Serikali
Katika kila awamu serikali imekuwa ikijitahidi kwa kiasi chake kutatua changamoto za walimu, kama vile kuboresha miundo mbinu na hivi juzi wameongeza mishahara, lakini haya yote hayatoshi kumaliza na kurejesha heshima ya mwalimu iliyopotea katika taifa hili, Yafuatayo ni mapendekezo ya nini serikali ikifanye ili kuinua hali ya kiuchumi ya walimu.

Moja, Kuwapa heshima walimu wanayo sitahili katika nchi hii, kwani wao ndio msingi wa taifa la kesho. Swali ni je? Wana wapaje heshima hii, kwa kuongeza mikopo nafuu kwa walimu yenye riba inayolipika (Yaani isiyomuumiza mwalimu), kutengenezewa mazingira rafiki ya kufundishia na malazi, pia kuongezewa mishahara kwani kiwango wanachopewa na kazi wanayo ifanya hakiendani hata kidogo.

Jambo lingine na la mwisho ni Serikali kufanya uchunguzi (utafiti) kwa kuweka mfumo maalum unao waruhusu wadau wa elimu, walimu na sekita binafsi kutoa mapendekezo na maoni juu ya kuinua hali ya walimu inchini. Na kuyatendea kazi yale mawazo na maoni yanayotolewa kupitia mfumo huo.

Mwisho, Wadau wa elimu na Sekta binafsi
Ili kuboresha maslahi na maisha ya walimu ni muhimu kuwepo kwa ushirikiano kati ya wadau wa elimu au sekita binafsi na serikali pamoja na walimu wenyewe katika kutatua changamoto zao, Ushirikiano huu unaweza kuwa katika kuchangia vifaa vya kutumia walimu mashuleni, ujenzi wa miundo mbinu ya walimu, hata pia wa kimawazo kwani Ustawi wa walimu Tanzania ni mafanikio pia ya hizi sekita binafsi, kwani wataalam wa baadae wa sekita hizi wanatengenezwa na kuandaliwa n waalimu.

"Ualimi sio wito ni taaluma yenye sifa na tija kwa taifa la Tanzania. Tukiwathamini waalimu tumeithaminisha Tanzania".

Imeandikwa na,
Jeremiah Yombo Wana.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom