100% posible. Na hii ndiyo design ya mwanzo ya ndoa aliyoweka Mungu. Wale wanaochagua miili yao kuitawala akili na siyo akili kuutawala mwili hawawezi. Maana asili ya mwili ni kuwaka tamaa na kutoridhika lakini Mungu amekupatia akili ya kuchagua jema na kuuadibisha mwili ufuate uamuzi wako wa busara.
Kutawaliwa na mwili ama mazingira (eti wanavaa nusu uchi, eti kila mtu anafanya) ni kudhalilisha uwezo wa akili yako kuamua kufanya yaliyo mema. Akili ndio inayoleta utu, akili yako ikitawaliwa na utu wako umetawaliwa na unakuwa mtumwa wa mwili ama mazingira.
Acheni akili iamue jambo jema na mwili ufuate maamuzi ya akili uone nani atashindwa kuwa mwaminifu.