UAMINIFU; Nguzo Muhimu Kwa Mafanikio Ya Biashara Yako

UAMINIFU; Nguzo Muhimu Kwa Mafanikio Ya Biashara Yako

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532

Picha ambayo watu wengi ambao hawapo kwenye biashara wanayo kuhusu biashara ni kwamba biashara ni sehemu ya kufaidika wakati wengine wanaumia. Huwa wanafikiri kwamba kwenye biashara unahitaji kuangalia faida tu bila ya kujali mambo mengine yanaendaje.

Kwa mtazamo wa aina hii, watu wengi wamekuwa wanaingia kwenye biashara, wanapata mafanikio ya muda mfupi lakini hawachukui muda wanapotea kabisa. Hakuna kitu muhimu kwenye biashara yenye mafanikio ya kudumu kama uaminifu. Biashara zote ambazo unaona zimefanikiwa zimejengwa kwenye misingi ya uaminifu.

Biashara chache zinazoonekana kuendeshwa bila ya uaminifu hupata faida mwanzoni lakini hazidumu. Hufa haraka sana na kupotea kabisa.

Kama umeamua kufanya biashara, jua ya kwamba uaminifu ni kitu ambacho huwezi kucheza nacho hata kidogo. Uaminifu ni nguzo muhimu sana kwenye biashara yako. kwa jinsi utakavyotunza uaminifu ndivyo utakavyoweza kudumu kwenye biashara na kufanikiwa pia.

Zifuatazo ni njia za kujijengea uaminifu kwenye biashara yako ili uweze kupata mafanikio ya kudumu.

1. Jenga uhusiano mzuri na wateja.
Hakikisha mteja anakuwa na mahusiano mazuri na biashara yako. Toa huduma bora sana kwa wateja, wajali wateja wanapopata changamoto na kuwa tayari kutatua changamoto ambazo mteja anapitia kwenye biashara yako. kwa njia hii mteja atakuamini na kukuona wewe ni rafiki yake wa karibu.

2. Tekeleza unachoahidi.
Kama unawaahidi wateja kitu hakikisha unakitekeleza. Hakuna kitu kinapoteza imani ya wateja kama kuahidi kwamba akija kwenye biashara yako atapata kitu fulani halafu asikipate. Jitahidi sana kutimiza kile ambacho umewaahidi wateja wako na watajenga uaminifu mkubwa kwako.

3. Nenda hatua ya ziada.
Mteja ana matarajio fulani kutoka kwenye biashara yako. kwa kuyapata anafurahi na kuendelea kuwa na wewe. Ila pia mtu mwingine anaweza kujua mteja wako anapata nini na yeye akaanza kutoa kile kile. Kuepuka hili kuwa na tabia ya kwenda hatua ya ziada. Jua kile ambacho mteja anatarajia na nenda hatua ya ziada, toa zaidi. Hakikisha mteja anapata kitu bora zaidi ya alichotarajia na atakuamini sana.

4. Usiangalie faida ya muda mfupi tu, angalia na muda mrefu.
Kuna uwezekano ukafika mahali ambapo ili kumridhisha mteja inabidi uingie hasara. Sasa kama wewe utakuwa unaangalia faida tu utashindwa kufanya hivyo kwa kuona huwezi kuingia hasara hiyo. Ila kama unaangalia faida ya muda mrefu, utajua ya kwamba kwa kumridhisha mteja leo, kesho ataendelea kuja. Hivyo hata ukiingia hasara leo, kesho na siku zijazi utaendelea kupata faida.

5. Jenga utamaduni huu kwenye biashara yako nzima.
Wewe tu kuwa mwaminifu halafu wafanyakazi wako wakawa sio waaminifu ni kazi bure. Utamaduni huu wa uaminifu unatakiwa kuwa kwenye kila mtu anayehusika na biashara yako. mteja anatakiwa kuwa na amani anapokuwa kwenye biashara yako akijua ya kwamba yuko kwenye mikono salama.

Kama unataka biashara yako ikue na kufikia mafanikio ya kudumu, basi nguzo kuu ni uaminifu. Ukikosa uaminifu hakuna atakayetaka kufanya biashara na wewe. Utapotea wateja na hata washirika wa kibiashara.



Kwa ushauri wa biashara piga simu 0713 666 445.
By Napenda Biashara
 
Ahsante ila kua mbunifu wa kuandika short and clear thread
 
Back
Top Bottom