Uaminifu unamweka mtu kwenye uangalizi wa karibu na Mungu

Uaminifu unamweka mtu kwenye uangalizi wa karibu na Mungu

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
557
Reaction score
858
Zab 101:6 SUV
[6] Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, Hao wakae nami. Yeye aendaye katika njia kamilifu, ndiye atakayenitumikia.

Kupitia andiko hili tunapata mtazamo wa Mungu juu ya wale ambao ni waaminifu na wanaoenenda katika njia kamili, watu wasio na kona mbele za Mungu, wameweka njia yao vizuri mbele zake.

Ahadi ya Mungu ipo wazi kwa watu waaminifu, ameahidi mwenyewe kuwaangalia kwa ukaribu, sio hivyo tu atawakaribia watu hao, na kuwapa nafasi ya kumtumikia yeye.

Kumbe ukiwa mwaminifu unapata kibali chake, ooh! kumbe wale watu ambao ni waaminifu sana mbele za Mungu, wanacho kibali kisicho cha kawaida, kwa kifupi huwezi kuwaharibia watu hawa, Mungu ameachilia kibali ambacho sio cha kujipendekeza kwa mtu yeyote, kinatoka kwake moja kwa moja.

Tuna somo kubwa sana la kujifunza hapa, kama mtumishi wetu mbele za Mungu ulikuwa wa kulega tunapaswa kuliweka sawa hili, maana tunakosa mambo mengi mazuri kutoka kwa Mungu.

Mtu aliye mwaminifu mbele za MUNGU atakuwa mwaminifu kwa wazazi wake, viongozi wake, mume/mke wake, atakuwa mtu bora katika biashara zake na kazi zake, ndani yake hana ubabaishaji, hatafuti sifa kwa watu, anafanya hayo kwa ajili ya kuendelea kumpendeza Mungu wake.

Kama kuna eneo la kufanyia kazi sasa ni kuanza kuwa mwaminifu mbele ya Mungu, kujitenga mbali na mambo yanayoharibu kazi yako, hutafanya hayo kwa ajili ya mtu, utafanya kwa ajili ya MUNGU wako, itakusaidia kuwaamini kweli.

Ikiwa mtu anaweza kukutana na uwepo wa Mungu zaidi kwa ukaribu, hatupaswi kupuuza fursa hii, tunapaswa kuishi maisha ambayo yamejaa kwake sirini na kwa uwazi itatusaidia kulinda uwepo wa Mungu uendelee kudumu katika maisha yetu.

Kinyume chake ukiwa sio mwaminifu mbele za MUNGU unaharibu uhusiano wako na Mungu, unakosa ule ukaribu wa Mungu katika maisha yako, jambo ambalo hupaswi kulitamani liwepo kwako.

Nitakuwa sijakutendea haki kama sitakukaribisha kwenye kundi hili zuri la wasap la kusoma biblia kila siku na kutafakari, ni moja ya kundi linaloweza kusoma kumjua Mungu wako vizuri kupitia neno lake. Ukipenda hili wasiliana nasi kwa wasap +255759808081 ili uweze kuunganishwa kwenye kundi hili zuri.

Mwisho, nikukaribishe kwenye chaneli ya wasap kupata mtu mbalimbali bonyeza kiungo hiki=>>Samson Ernest | WhatsApp Channel

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Back
Top Bottom