Uamsho wachomoka

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,575
MPANGO wa kuwabadilishia hati ya mashtaka viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (Jumiki) umekwama baada ya mahakama kutupilia mbali ombi la upande wa mashtaka katika kesi hiyo.

Ombi la kubadilisha hati ya mashtaka liliwasilishwa katika mahakama ya wilaya Mwanakwerekwe na mawakili wa washtakiwa na kupingwa vikali na mwendesha mashtaka wa serikali, Mohamed Ali Mohamed, juzi.

Akisoma hukumu yake, Hakimu Khamis Jafari, alisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili katika kesi hiyo ameona hakuna sababu za msingi za kubadilisha hati ya mashtaka dhidi ya viongozi wa Jumiki, Zanzibar.
Hakimu Khamis alisema kwa msingi huo kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kama kawaida kwa kutumia hati ya mashtaka iliyokuwa imefunguliwa mwanzo Aprili mwaka jana.

"Sioni sababu za msingi za kubadilisha hati ya mashtaka baada ya kusikiliza hoja za pande mbili katika kesi hii," alisema.

Hata hivyo mwendesha mashtaka, Mohamed Ali Mohamed, hakukubaliana na uamuzi huo na hivyo kukusudia kukata rufaa kupinga uamuzi huo.

Washtakiwa saba katika kesi hiyo wamefunguliwa mashtaka ya kufanya mkusanyiko usio halali kinyume na sheria Na. 6 ya mwaka 2004 ya mwenendo wa makosa ya jinai ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, viongozi hao wanadaiwa kuwa saa 6.30 mchana wa Mei 26 mwaka jana walifanya mkusanyiko usio halali na kuandamana kinyume cha sheria.

Washtakiwa hao ni Sheikh Farid Hadi Ahmed, Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Abdalla Saidi Ali Fikirini Majaliwa Fikirini, Mbarouk Saidi Khalfan, na Haji Sadifa Haji.

Washtakiwa hao wanatetewa na wakili mkongwe wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Salum Toufiq na Abdalla Juma ‘Kaka', ambapo kesi hiyo imepangwa kutajwa tena Machi 28, mwaka huu.

Wanaswa kwa uchochezi


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kujihusisha na uchochezi wa kidini na kusababisha uvunjifu wa amani na umwagaji damu baina ya dini na dini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Suleimana Kova, alisema kuwa watu hao wamekamatwa katika msako maalumu wa kukabiliana na uchochezi wa kidini.

Alisema kuwa uchochezi wa kidini umesababisha machafuko nchini hadi kuuawa kwa baadhi ya viongozi wa dini na wengine kujeruhiwa hali inayosababisha hofu kubwa kwa jamii kuishi bila amani.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Kombo Zuberi (32) mkazi wa Mburahati, Basote Tandala @ Rayan mkazi wa Gongo la Mboto (24), Mohamed Sharif (33) mkazi wa Tabata Bima, na Salum Mahambi (46) mkazi wa Tunduma.

Kova alibainisha kuwa mtuhumiwa Kombo ni kati ya watuhumiwa wanne ambao walitakiwa kujisalimisha lakini aliendelea kubaki mafichoni hadi alipokamatwa hivi karibuni na kwamba ndiye kiongozi wa uchochezi.

"Huyu mtuhumiwa amekutwa na nyaraka nyingi za aina mbalimbali alizokuwa akisambaza yeye na wenzake hapa jijini na mikoani kwa makusudi ya kuleta mfarakano wa kidini nchini huku nyingine zikichochea chuki na vurugu dhidi ya serikali na taasisi nyingine," alisema.

Kova alisema kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya wakili wa serikali kupitia jalada la kesi hiyo na kuthibitisha kiwango cha tuhuma hizo kilingana na makosa yatakayobainika.

[TD="bgcolor: #ffffff"]
[/TD]
[TD="align: center"][/TD]
 
Mwezi mungu watoe uamsho kwani wamefungwa kwaajiri ya kuupinga muungano,nasio udini nimeangaria cd zao nyingi jamaa hawautaki muungano na muda utakapo jiri itakua open
 
LET THEM FREE,vyovyote iwavyo source kubwa ya mapambano yao ni MUUNGANO.
 
Sioni sababu za msingi za kubadilisha hati ya mashtaka baada ya kusikiliza hoja za pande mbili katika kesi hii," Haya ni majungu tu heshimu mamlaka yaliyowekwa duniani na juu pia siyo kuja humu kujenga hoja ambazo hazina mashiko
 
Mwendesha mashitaka wa ..........nae itafika siku yake atakutana na mwendesha mashitaka wa mwenyezi Mungu. Maisha ya dunia ni mafupi sana.
 
Nawaagiza FBI wakamchunguze huyo hakimu..
La abadilishwe wamchukue kutoka bara
 
Mwezi mungu watoe uamsho kwani wamefungwa kwaajri iya kuupinga muungano,nasio udini nimeangaria cd zao nyingi jamaa hawautaki muungano na muda utakapo jiri itakua open
ri kosa li sawa
 
Mungu ndie hakimu wa wote,iko cku ukweli utacmama haiwi firauni aliwauwa watoto wa kiume wa kiizraili kuogopa kuangushwa utawala wake na bado haki ikasisima, kuwaweka watu ndani sio dawa ya kuficha ukweli na uchafu huondoshwa sio kuficha chini kapati unajidanganya.
 
Mwezi mungu watoe uamsho kwani wamefungwa kwaajiri ya kuupinga muungano,nasio udini nimeangaria cd zao nyingi jamaa hawautaki muungano na muda utakapo jiri itakua open
sahihi kabisa,hawa jamaa sio walikuwa wanapinga dini nyingine hapana walikuwa wanapinga muungano
 
:iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…