KALYANKOZILE
Member
- Apr 24, 2013
- 19
- 1
Dodoma. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa ameelezea kukerwa na daraja la tano katika muundo mpya wa kupanga matokeo, kuitwa sifuri.
Dk. Shukuru Kawambwa, aliyasema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alivishutumu vyombo vya habari kwa kuchanganya alama na madaraja yaliyopo katika muundo mpya wa kupanga matokeo ya mitihani nchini.
Alisema kwa muundo mpya, daraja sifuri ni kati ya pointi 48 na 49 ambayo inapatikana baada ya mtahiniwa kupata alama F kwa masomo yote saba.
Ndugu zangu waandishi wa habari, kitu ambacho hamkufanya haki kwa Watanzania safari hii, ni ile kuliita daraja la tano kuwa ni sifuri mkalazimisha na mimi kumwagiza Katibu Mkuu abadilishe na kuita daraja sifuri,alisema D.k Shukuru Kawambwa.
CHANZO:Gazeti la mwanachi Marchi 2,2014
Ushauri wangu kwako ,Kiongozi lazima awe na msimamo wa kufanya maamuzi yenye manufaa kwa taifa na sio kusema nimelazimishwa au kulazimishwa.Hii inadhiilisha wazi wazi kuwa una udhaifu katika utendaji wa shughuli zako ndio maana kila mwaka watanzania tunabakia kujadili daraja sifuri.Hivyo nakuomba ujitafakari na kuanza kubadilika ili elimu yetu iwe na ubora na ndipo watanzania tutasema sasa ni "BIG RESULT NOW" kuliko ilivyo sasa "MATOKEO MABAYA SASA"
KWA PAMOJA TUTALIJENGA TAIFA LA TANZANIA.