katika harakati zangu za kuwa mjasiriamali nikajikusanyia ka mtaji ambako hadi sasa kamefikia milioni 4. nilikuwa najikusanyia kwa kudunduliza kamshahara na biashara za mkononi. wakati najikusanyia hiyo fedha mkakopa benki nkanunua kiwanja. sasa nikiangalia hiyo 4m haitoshi hata kujenga nyumba na nilikuwa nimepanga kufanyia biashara hapa nilipo ila gharama za kupata sehemu ya biashara zimekuwa kubwa na hivyo nimeona ninunue tu kiwanja kingine hapa nilipo ila bado sijafanya hivyo. Naomba ushauri ni sahihi kununua kiwanja kingine au kujenga nyumba ambayo haitamalizika? fedha naipata taratibu sana. naamini ma thinkers mtanipa ushauri mzuri na Mungu awabariki