LGE2024 Uandikishaji Daftari la Wapiga Kura umefanyika kihuni Halmashauri ya Songea. Baadhi ya wananchi wameandikiana majina

LGE2024 Uandikishaji Daftari la Wapiga Kura umefanyika kihuni Halmashauri ya Songea. Baadhi ya wananchi wameandikiana majina

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Joined
Sep 23, 2024
Posts
64
Reaction score
43
Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa umefanywa ‘kihuni sana’ hapa Songea

Moja ya changamoto kubwa ambayo niliiona katika mchakato wa Uandikishaji Wapiga Kura katika Daftari kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mtaa ni Wananchi wengi kukosa elimu ya mchakato huo, hilo likachangia mambo mengi kwenda ndivyo sivyo, katika lugha nyepesi mambo mengi yameenda ‘kihuni’.

Mimi ni mkazi wa Halmashauri Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma, huku kwetu nimeshuhudia michezo mingi michafu ya kisiasa katika mbio za kutafuta uongozi.

Kuandikiana majina kinyume cha utaratibu. Suala la Watu kuandikiana majina, yaani fulani akiwa hayupo na wanajua ni Mwananchi au mkazi wa eneo husika kuna mtu anajitokeza anamuandikia jina na kumsainia pia.
Kituo kimoja wapo cha Kata ya Matarawe ,nilikaa nyumba ya jirani kwa Muda wa nusu Saa sikushuh...jpg

WhatsApp Image 2024-10-21 at 19.24.52_dc668a5d.jpg
Jambo lingine ni kuwa wapiga kura waliokuwa Wagonjwa nao wanaandikiwa kwenye listi ya Wapiga kura, hilo limefanyika kwa sana tu.

Kuna baadhi ya viongozi ambao wanainjinia mchezo huo kwa kuwapa fedha makada ili wakaandike majina hayo mitaani chini ya usimamizi wa Kigogo mmoja ambaye mwenye wadhifa ndani ya Baraza la Mawaziri, wenyeji watakuwa wamenielewa.

Moja ya sababu ya hayo yote kutokea ni kwa kuwa mchakato wa uandikishaji wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi huo, elimu haikutolewa vya kutosha, Wananchi wengi wa kawaida hawaelewi wanachotakiwa kufanya na umuhimu wake.

Kuna baadhi nilipokuwa nazungumza nao hawajui hata wanajiandikisha ili wapige kura kwa ngazi gani, wanafikiri inahusiana na uchaguzi mkuu pia.

Wengine ambao sio wafuatiliaji wa vyombo vya habari walikuwa hawajui zoezi limeanza lini na linaisha lini, unakutana na swali kwani mwisho lini?
WhatsApp Image 2024-10-21 at 19.18.07_cc711938.jpg
Wengine wanajiandikisha popote
Kingine ambacho kimetokea ni Wananchi kujiandikisha katika kituo chochote ambacho anaona yupo karibu nacho kwa wakati huo au kwa kufuata maelekezo ya kiongozi fulani ambaye ana manufaa naye bila kujua ni kinyume cha utaratibu.

Mfano kuna kituo kipo Kata ya Mshangano, Mtaa wa Namanyigu “Kwa Lipepe” wanaotakiwa kuandikishwa pale ni wakazi wa Mtaa wa Kuchile, Kata ya Seedfarm lakini nimeshuhudia wakazi wa mitaa miwili tofauti kutoka kata mbili tofauti wakijiandikisha pale akiwemo mzee mwenyewe mwenye Jina la KWA LIPEPE nae amejiandikisha katika kituo hicho badala ya kituo alichotakiwa kujiandikisha cha Kidodi Kata yake ya Mshangano.

Wanaojiandikisha ni wale wa kutoka Kata ya Mshangano, Mtaa wa Namanyigu na wa kutoka Kata ya Seedfarm Mtaa wa kuchile.

Viongozi wa mtaa wanalijua hilo ila kwa makusudi wanaacha iwe hivyo.

Kwa hiyo ni kituo kilichowekwa kwa ajili ya kuiba wapiga kura wa eneo hilo. Kituo kimewekwa nyumbani kwa mtu ni hatua chache toka kwa balozi halali wa eneo hilo (mama Mbuli) ambaye ni wa Kata ya Mshangano.

Wengine wanasombwa tu Kwa shinikizo la kiongozi wa mtaa.
Kulikuwa na wimbi la baadhi ya viongozi kukusanya wapiga kura kuwapeleka kwenye vituo na sio kuwaelimisha, matokeo yake wengi tu wakawa wanajiandikisha kama nilivyosema hapo juu katika vituo ambavyo haviwahusu.

Wengine wanadanganywa fursa ya Mikopo. Kumekuwa na baadhi ya Viongozi kwa sababu wanazozijua wao wanawadanganya Wananchi kuwa wanapojiandikisha kwenye madaftari ya kupiga kura watakuwa na nafasi nzuri ya kupata mikopo kirahisi.

Wengine wanawazungukia Wazee
Baadhi ya Makada wa Chama wanawazungikia Wazee na Wagonjwa kuandika majina yao na kuyapeleka kwenye kituo kuorodhesha na kughushi sahihi kitu ambacho si sahihi kwa mujibu wa muongozo.

Usalama wa Daftari ni mdogo
Watu wamejiandikisha lakini mazingira ya usalama wa Daftari la Wapiga Kura ni mdogo, kama wanaweza kubeba majina na kwenda kuyaandika wenyewe kwenye daftari, bila shaka kuna michezo mingi michafu imefanyika kwenye daftari hilo.

Kwa mazingira hayo ilipokuwa inafika jioni vituo vinafungwa daftari anaondoka nalo msimamizi msaidizi ni wazi kuwa kuna mengi yamefanyika huko anakoenda nalo.

Wapinzani nao wamo
Katibu Mwenezi wa Jimbo la Songea mjini wa CHADEMA naye katika eneo lake analoishi la Kata ya Lizaboni alinukuliwa sehemu akisema wao waliweka mawakala 10 kati ya Vituo 21, akawa analalamika wanachofanyiwa na wapinzani wao sio kitu kizuri.

Alidai kwa vile vituo ambavyo hawajaweka mawakala kuna michezo mingi ya kihuni inafanyika ila hawakukata tamaa wakaendelea kuhamasisha watu wakajiandikishe na matokeo yataonekana mbele ya safari pale atakapochaguliwa kiongozi ambaye wananchi hawajamchagua kwasababu atakosa ushirikiano katika uongozi wake.

Kwa maoni yangu kama iko hivi, ni bora wangetumia njia ya uandikishaji wa nyumba kwa nyumba kama ule utaratibu wa sensa na sio kukaa kwenye Vituo ambavyo tunashuhudia muitikio wa wananchi ni mdogo
Wanaamini kutakuwa na wapiga kura wengi wa kupikwa.
 
Hivi, mimi ndio sijui au nimechelewa kujua? Kwani, hata wangeandikisha wenye sifa nchi nzima, tatizo liko wapi?
Kinachopaswa kupewa uzito ni uandikishaji au upigaji kura?
 
Walimu ,watendaji vijiji walipelekewa majina wajaze yaani wizi juu ya wizi Leo nimepita vituo kama vinne CCM walikuwa wanafanya uchaguzi nilichokiona ni balaa Raia wamepigana hatareeeee hadi ilibidi kituo kimoja waite polisi ,ccm ni weziiiiiiiiiiiiiii
 
Hivi, mimi ndio sijui au nimechelewa kujua? Kwani, hata wangeandikisha wenye sifa nchi nzima, tatizo liko wapi?
Kinachopaswa kupewa uzito ni uandikishaji au upigaji kura

Hivi, mimi ndio sijui au nimechelewa kujua? Kwani, hata wangeandikisha wenye sifa nchi nzima, tatizo liko wapi?
Kinachopaswa kupewa uzito ni uandikishaji au upigaji kura?
Uzito mkubwa upo kwenye uandikishaji, kwasababu hiyo ndio sifa mojawapo ya kumpigia kura kiongozi umpendae
 
Tuangalie picha kubwa zaidi nayo ni mchakato wa kupiga kura. Je, kama ni kweli kuna watu wameandikiwa majina na wenzao pia watawapigia kura? Kwa sababu kwa vyovyote vile HAIWEZEKANI kupigiana kura, alama ya wino kwenye dole gumba itakuhukumu
 
Tuangalie picha kubwa zaidi nayo ni mchakato wa kupiga kura. Je, kama ni kweli kuna watu wameandikiwa majina na wenzao pia watawapigia kura? Kwa sababu kwa vyovyote vile HAIWEZEKANI kupigiana kura, alama ya wino kwenye dole gumba itakuhukumu
Hapo ndipo Goli la mkono linapotokeaga, kila Jina Ni Kura kitakachoangaliwa idadi isivuke ya waliojiandikisha.
 
Back
Top Bottom