LGE2024 Uandikishaji katika Kata ya Sinoni ulitawaliwa na kuandika majina bandia, wanadai ni maelekezo kutoka juu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Mimi ni wakala na kiongozi wa CHADEMA cha siasa hapa Arusha, Kata ya Sinoni, Mtaa Engosingiu.

Wakati wa zoezi la uandikishaji hapa Mtaa wa Engosingiu na Mlimani linaendelea nimegundua kuna namna fulani waandikishaji wanafanya hila na udamnganyifu hasa katika eneo kama letu ambako upinzani umechachamaa.

Wakati zoezi la uandikishaji linaanza mchakato ulifanyika vizuri kuanzia tarehe 11 na 12 lakini kuanzia siku ya tatu kulianza kutokea mauzauza mengi ikiwemo CCM kutuzuia mawakala kujua idadi ya Watu walioandikishwa kwa siku.

Mbaya zaidi nimegundua kuwa ukiondoka hata na hesabu kesho yake unakuta imeongezeka. Tuseme leo tumefunga na watu waliojiandikisha ni 200 kesho asubuhi unakuta wameongezeka hadi 300.

Hali hii imenipa maswali mengi kwani ukijaribu kuongea na karani anakwambia ni maelekezo kutoka kwa msimamizi wao na hata tulivyoongea na mtendaji anasema atashughulikia lakini hakuna chochote kinachofanyika.

Baada ya kuzungumza nao wanasema kuwa wamepewa maelekezo, sasa najiuliza wanafuata maelekezo au kanuni za Uchaguzi?
 
Nape hakukosea,ingawa cheo amekikosa!
 
aya sio sinoni tu sehemu nyingi walielekezwa kufanya hivo,unalazimishwa ulete majina 200 na huku umeandika themanini maelekezo ni kwamba ukiweza nenda na daftari home changanya hayo majina rudia na mengine,weka sahihi za initials tu ili mradi idadi itimie
 
Back
Top Bottom