LGE2024 Uandikishaji Uchaguzi Serikali za Mitaa unaruhusu mtu kujiandikisha mara nyingi awezavyo, ni mbinu ya kuruhusu wizi wa kura?

LGE2024 Uandikishaji Uchaguzi Serikali za Mitaa unaruhusu mtu kujiandikisha mara nyingi awezavyo, ni mbinu ya kuruhusu wizi wa kura?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu salam,

Leo nilipanga kwenda kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa, na kweli nimefanya hivyo.

Ukienda kujiandikisha unakuta mwandikishaji yuko na daftari ambako unaulizwa jina na umri pekee kisha unasaini, na mtu huyo atakwambia majina yatabandikwa uje kuhakiki, na kukukaribisha kupiga kura siku ya tar 27 Novemba, 2024.

Kwa lengo la majaribio nikasema ngoja nitafute sehemu nyingine kama nitaulizwa kitu kingine zaidi ya hiki, nimefika hapo ni hivyo hivyo.

Hii inamaanisha kama una muda unaweza kupitia kwenye vituo zaidi ya 20 kwa siku!

Ni loophole kubwa sababu ya kutumia makaratasi. Kwanini mfumo wa kidogitali hautumiki ili kama mtu kajiandikisha sehemu moja system ioneshe huyu ameshajiandikisha?

Kama watu wanalipa machawa kuwasifia watashindwa hapa kulipa watu kwenda kujiandikisha ambako hahusiki?

Wizi ule wa sanduku umegoma sasa mmekuja na uvumbuzi mpya! OR TAMISEMI mna lipi la kusema kwenye hili?
 
Ukiona wazungu wanatuita manyani ujue hawakosei. Hizo ndio sababu zinazopelekea wao kufikia hitimisho hilo.
 
Back
Top Bottom