Martha Magawa
New Member
- May 7, 2024
- 1
- 0
Na Mwandishi wetu.
Wanahabari wenye weledi na wanaozingatia maslahi ya Taifa ni chachu ya kutimiza dhima ya kuleta mchango kwa taifa.
Haiba na taswira yenu nzuri huwa inaharibiwa na uandishi wa habari usiofuata maadili ya uandishi wa habari, kuandika habari ambazo hazijafanyiwa utafiti, kuandika habari za uongo na za kupotosha zenye lengo la kuichafua Serikali au mtu mmoja mmoja ambazo tumeziona zikiharibu na kuchafua kabisa taaluma ya habari miaka ya hivi karibuni.
Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari, hili tutajadili siku nyingine lakini uhuru huu uwe na mipaka, tumieni misingi ya taaluma ya habari katika uandishi mkizingatia miiko ya uandishi wa habari mnazowapelekea wananchi, msiweke mawazo yenu wenyewe katika uhabarishaji, msitumie hisia wala kutumika kukamilisha ‘mission’ za Watu wengine.
Taaluma imekuwa daraja la Watu kukamilisha Ajenda zao kupitia mwamvuli wa uandishi wa habari, sio dhambi Mwandishi wa habari akiwa Kiongozi yeyote wa siasa lakini isiwe mazoea na Watu kutumia mlango huo kwani unapelekea kuharibu taaluma, Waandishi wa habari na vyombo vya habari ni daraja kati ya wananchi na Serikali.
Wananchi wameviamini vyombo vya habari wakiamini ndio sauti zao watawasemea changamoto yao, lakini imekuwa tofauti sasa hivi ni mwendo wa kusifu na ‘kuabudu’ anayekosoa anaonekana hafai na mpinzani wa serikali iliyopo madarakani.
Wako wapi waasisi wa Taaluma hii? Liko wapi Jukwaa la Wahariri TEF? Liko wapi Baraza la Habari MCT? Wote hawa ni kweli wameruhusu Uandishi kuwa ‘mission’?
Waandishi wanawapambania wengine ikiwa wao wamejisahau na kujitoa sehemu ya wananchi, hawahoji tena maswali magumu na yenye tija kwa viongozi, wamekuwa wapokea taarifa na sio kuzitafuta taarifa.
MIKATABA YA KIMATAIFA
Misingi ya sheria na sera mbalimbali ya Kimataifa, bara na Nchi inalinda tasnia ya habari, Waandishi wa habari na Serikali. Mikataba hiyo inaweka wajibu kwa Serikali kufuata kuendeleza na kulinda Uhuru wa kutoa maoni na kujieleza.
Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu (UDHR)
Kifungu cha 19 cha Tamko hilo kinasema: Kila Mtu ana haki ya uhuru wa kutoa maoni na kujieleza; haki hii pia inahusisha uhuru wa Mtu kuamini katika maoni yake bila kuingiliwa kwa namna yoyote na uhuru wa kutafuta na kusambaza taarifa, maoni na mawazo yake kwa njia yoyote bila kujali mipaka.
Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR)
Tanzania imeridhia mkataba huu mwaka 1976 na hivyo inawajibika kisheria kufuata masharti ya mkataba huo. Kifungu cha 19 cha mkataba huo kinazungumzia Uhuru na haki ya kujieleza.
1. Kila Mtu atakuwa na haki ya kuwa maoni na kuyaamini maoni hayo bila ya kuingiliwa kwa namna yoyote.
2. Kila mtu atakuwa na haki na uhuru wa kujieleza; haki hii itahusisha mtu kutafuta, kupokea na kusambaza taarifa au mawazo ya aina mbalimbali kwa njia ya mdomo au maandishi na bila ya kujali mipaka kwa kuandika au kuchapisha kwa njia ya sanaa au njia nyingine yoyote akatayochagua.
Vikwazo kwa uhuru wa kujieleza vilivyoanishwa kwenye kifungu cha 19 vitakubalika kisheria iwapo vitakidhi masharti ya jaribio jumuishi lenye sehemu tatu kama ilivyooneshwa kwenye kifungu cha 19(3)
a) Kikwazo chochote ni lazima kiwekwe kwa mujibu wa sheria ambayo iko wazi na inayoweza kuonwa na kila mtu (kanuni za uwazi na kutabirika);
b) Kikwazo chochote ni sharti kiendane na moja kati ya malengo ya kifungu cha 19(3) ambayo ni
I)Kulinda haki na heshima ya Watu wengine;
II) kulinda usalama wa nchi au utulivu wa kijamii au afya na maadili ya jamii
MIKATABA YA BARANI AFRIKA
Mkataba wa Haki za Binadamu na Haki za Watu wa Umoja wa Afrika (Mkataba wa Afrika)
Kifungu cha 9 cha Mkataba wa Afrika kinalinda haki ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni:
1. Kila mtu atakuwa na haki ya kupokea taarifa.
2. Kila mtu atakuwa na haki ya kujieleza na kusambaza mawazo yake kwa kuzingatia misingi ya sheria.
Tume ya Haki za Binadamu na Haki za Watu ya Umoja wa Afrika (ACHPR) ina wajibu wa kufasiri Mkataba huo.
Tume hiyo imekuwa ikitekeleza wajibu huo kwa namna
mbalimbali, ikiwemo njia ya kutoa Maazimio na Matamko.
Maazimio na Matamko ya Msingi ya ACHPR;
Azimio Kuhusu Haki ya Uhuru wa Taarifa na Kujieleza Kupitia Teknolojia ya Intaneti Barani Afrika (lilikubaliwa Tarehe 4 Novemba 2016): Nchi zilizoridhia Mkataba wa Afrika hazina budi kutunga
Sheria zitakazohakikisha kupatikana, kuheshimu na kulinda haki ya wananchi ya uhuru wa taarifa na kujieleza kwa kupitia teknolojia ya intaneti.
Azimio Kuhusu Usalama wa Waandishi na Watendaji Wengine wa Tasnia ya Habari (hikubaliwa Tarehe 12 Mei 2011): Nchi (na mamlaka zake husika) zilizoridhia Mkataba wa Afrika hazina budi kutekeleza wajibu wao wa kuzuia na kuchunguza matukio yote ya uhalifu dhidi ya waandishi au watendaji wengine wa tasnia ya habari na kuwashughulikia wahusika wote.
KATIBA YA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalinda uhuru wa kujieleza, japokuwa haielezi moja kwa moja kuhusu uhuru wa vyombo vya habari:
Kila mtu -
(a)ana uhuru wa kuwa na maoni na kujueleza maoni au mawazo yake;
(b) ana haki ya kutafuta, kupokea na, au kusambaza taarifa bila ya kujali mipaka ya nchi;
(c) ana uhuru wa kuwasiliana na haki ya kulindwa dhidi ya kuingiliwa kati kwa mawasiliano yake; na
(d)ana haki ya kupata taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu yanayoendelea kuhusu maisha na
shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu.
MIPAKA
Haki hizi za Kikatiba, ikiwemo Ibara ya 18, hazitatumiwa au kutekelezwa na mtu mmoja kwa namna ambayo itazuia
au kuingilia kati uhuru wa watu wengine, au maslahi ya umma (Ibara 30(1)). Haki hizi zinzaweza kuzuiwa kwa sababu mbalimbali:
• Kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango ya mandeleo ya miji na vijiji, ukuzaji
namatumiziyamadiniauukuzajinauendelezaji wa mali au maslahi mengineyo yoyote kwa nia ya kukuza manufaa ya umma; au
• Kulinda heshima, haki na uhuru wa watu wengine au faragha ya watu wanaohusika shauri lolote mahakamani, kuzuia kutoa habari za siri, au kutunza heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama.
Muhimu: Masharti haya ni mapana kuliko yaliyoainishwa kwenye Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR).
Kwa kuzingatia maudhui ya Katiba,
kanuni za uwiano na umuhimu hazipewi uzito unaostahili kama vigezo muhimu katika kuzuia haki hizi za msingi.
SHERIA ZA NCHI ZA UDHIBITI WA VYOMBO VYA HABARI
Sheria ya Huduma za Habari, 2016
Sheria ya Huduma za Habari inasimamia weledi katika tasnia ya habari, na inaunda Bodi ya Ithibati ya Wanahabari, Baraza Huru la Habari, na Habari na misingi mingine ya udhibiti wa tasnia ya habari.
Vipengele muhimu na athari zake kwa tasnia ya habari ni pamoja na:
Usajili na Ithibati:
Vyombo vya habari vya uchapishaji (magazeti)
vinalazimika kupata
leseni kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.
Kifungu cha 8-10 vinaeleza mchakato wa kuomba, kukataliwa, na kufutwa kwa maombi ya leseni. Mamlaka ya rufaa dhidi ya maamuzi hayo yapo chini ya Waziri mwenye dhamana ya maudhui na rufaa inalazimika kuwasilishwa ndani ya siku thelethini baada ya kutolewa kwa uamuzi husika.
Sheria hii pia inaweka masharti ya mwandishi wa habari kuthibitishwa (kupata ithibati) ili kufanya kazi za uandishi. [Kifungu cha 19] Bodi inaweza kufuta uthibitisho wa mwanahabari kutokana na kukiuka kwa kiasi kikubwa maadili ya taaluma yaliyoainishwa katika kanuni za maadili ya taaluma ya uandishi wa habari, na kwa mwandishi wahabari asiye raia wa Tanzania, kutotekeleza lengo la uthibitisho wake.
Bodi hutunza orodha ya wanahabari ikijumuisha majina na maelezo ya wanahabari
waliothibitishwa.
• Mwandishi ambaye jina lake limeondolewa kutoka kwenye Orodha ya Wanahabari au
aliyesimamishwa kufanya kazi za uandishi wa habari hatofanya kazi hizo walau kwa muda wa miezi mitatu.
Mamlaka ya rufaa dhidi ya maamuzi hayo yapo chini ya Waziri na Mahakama Kuu. [Kifungu cha 21]
Athari: Hitaji la kisheria la kusajili na kutoa ithibati kwa waandishi wa habari lina changamoto kubwa, kwa kuwa ni kikwazo kwa watu waaandishi wanaopenda ama kuhitaji kuingia wenye taaluma hiyo.
Mamlaka mbalimbali zinapewa madaraka kubwa katika kudhibiti maudhui na shughuli za kila siku za vyombo vya habari.
Nguvu hizo, hasa kwa vyombo binafsi vya habari, zinaingilia uhuru wao wa uhariri na hivyo kuathiri kwa upana uhuru wa vyombo vya habari, kutoa maoni na kujieleza.
Zaidi ya hapo, jamii inanyimwa haki yake ya kupata taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari na maoni aina mbalimbali za maoni.
Mamlaka ya Polisi
Jeshi la Polisi limepewa mamlaka pana ya kufanya upekuzi kwenye chombo cha habari na kukamata kifaa chochote kilichoanzishwa, kuwekwa, au kuendeshwa kwa kukiuka matakwa ya Sheria hii. [Kifungu cha 60]
Makosa chini ya Sheria Hii
• Kifungu cha so cha Sheria hii kinaeleza makosa na adhabu kwa kuchapisha habari kwa makusudi, uzembe, ya kutungwa na ya ongo, yenye nia ovu au ya kutungwa na ya uongo; au taarifa iliyokatazwa inayoweza kuhatarisha maslahi ya jamii, na hadhi, haki au uhuru wa watu wengine.
• Makosa mengine ni pamoja na kuendesha chombo cha habari bila ya kuwa na leseni, kufanya kazi ya uandishi wa habari bila ya kuthibitishwa na mamlaka husika, au kusambaza taarifa za uongo na zisizothibitishwa.
• Makosa yanayohusu kashfa pia yameainishwa kwenye Sheria hii. Hairuhusiwi kuchapisha
ama kutangaza habari zenye kukashifu.
Baada ya kuzipitia sheria hizi nini kifanyike?
Kuna haja ya wadau mbalimbali wa tasnia ya habari kukutana na kujadiliana juu ya utekelezaji wa kanuni ya sharia za huduma za vyombo vya habari inayomtaka mwanahabari kuwa na elimu ngazi ya diploma na kuendelea kwa ajili ya fani hiyo.
Lakini pia kwa kuzingatia maslahi ya malipo ya wanahabari ili kuepukana na rushwa hasa kutoka kwa wanasiasa.
Vituo vya habari vimejificha katika mwamvuli wa kutumia waandishi wa kujitolea na mikataba yenye malipo duni kiasi cha kutokidhi mahitaji yao ya kila siku.
Ugumu wa maisha umewalazimu baadhi ya waandishi kuwa chawa kwa viongozi na wadau mbalimbali wanaohitaji mkono wa vyombo vya habari katika kufanikisha malengo hayo. Nyakati za uchaguzi zinazungumza mengi juu ya hili kwani viongozi wengi wa vyama vya siasa hujishikamanisha na waandishi wa habari kama daraja la kukamilisha ‘mission’ zao.
Tafiti iliyochapishwa katika jarida la The Richest inataja katika taaluma kumi zisizoaminika ulimwenguni namba nane na sita zinashikiliwa na vyombo vya habari na nafasi ya pili ikishikiliwa na wanasiasa.
Inaelezwa kuwa uhusiano uliopo baina ya vyombo vya habari na wanasiasa ndio uliochangia kutokuaminika kwa tasnia ya habari.

Upvote
1