Uandishi wa barua za kiofisi

ntagunga

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Posts
704
Reaction score
285
Wana bodi heshima kwenu.

Wakati nafuatilia mchakato wa uhamisho, nimekutana na somo tajwa hapo juu, hali iliyopelekea kuleta hoja hapa ukumbini ili tuwe na mjadala wa wazi mwisho wa siku tuwe na maono sawa juu ya mada tajwa. Sehemu ya kwanza, ya mwandishi kumwandikia mkuu naamini haina shida sana ila mkuu kumwandikia mtumishi na kupitia kwa watu kadhaa ndo kuna mtihani.

Ili kufanikisha hili, naomba nitoe swali, ambapo kwa kila atakayejibu, ninachoomba ili kutokuwa na mlolongo mwingi, tujikite kwenye format tuu(namna inavyoandikwa) bila kuaandika barua yenyewe. Majibu yetu yahusishe anuani pekee na kichwa cha barua tu.

SWALI.
1(a). Wewe ni mwalimu, upo halimshauri ya wilaya ya kongwa, andika barua ya kuomba kuhamia halimashauri ya Bahi. Kumbuka barua yako ipitie kwa Mkuu wako wa shule, Afisa elimu wako na mkurugenzi wako wa halimashauri ya wilaya ya Kongwa.

(b) Wewe ni mkurugenzi wa Halimashauri ya bahi, mjibu mwalimu huyo kuwa ombi lake limekubaliwa.

NB. Ili twende sawa, ntakuwa najibu baadhi ya wachangiaji kwa "reply with quote" lakini baada ya kuridhika na michango ya wadau wote, nitakuja na hitimisho la somo hili kwa ku edit original post ili hata kwa atakayekuwa hajafuatilia mjadala, basi akisoma apate elimu hii.

Karibuni wana jukwaa. Unaeza kujibu kwa kiswahili au kiingereza.

NB: Ikumbukwe kuwa, siombi kufundishwa namna ya kuandika barua hizo, kwa mchakato niliopitia kuna kitu nimekipata kilichotofauti kabisa na nilivyokuwa najua. Hivyo jibu swali tu mwisho wa siku tutafundishana jambo la msingi ambalo napenda litubadilishe katika uandishi wa barua.
 
Duh....

Kwa ushauri wangu ingia google au youtube kuna maelekezo mengii tu hadi video clips kuanzia barua za malovee hadi za kiofisi.....

Kwa hapa sidhani kama watu watakupa ushirikiano ukizingatia na namna ya hitaji lako ulivyoliweka.

Goodluck.
 
Duh....

Kwa ushauri wangu ingia google au youtube kuna maelekezo mengii tu hadi video clips kuanzia barua za malovee hadi za kiofisi.....

Kwa hapa sidhani kama watu watakupa ushirikiano ukizingatia na namna ya hitaji lako ulivyoliweka.

Goodluck.

Mkuu tafadhali rejea swali vizuri, nimerekebisha na naomba mchango wako tafadhali Kizzy Wizzy


 
Formating iliyozoeleka nijuavyo ni kama ifuatavyo:-

Anuani ya mwandishi na tarehe kwa chini upande wa kulia mwa barua.

kushoto kwa barua ni yafuatayo

Kumbu namba ya barua inakuwa sambamba na tarehe

Anuani ya mkurugenzi wa bahi

K.K-Afisa elimu (m) Bahi
K.K-Mkurugenzi Kongwa
K.K-Afisa elimu (m) Kongwa
K.k. Mwl. Mkuu shule ya Kongwa

YAH: KUOMBA NAFASI YA KUFUNDISHA KATIKA HALIMASHAURI YAKO.


Sehem A nimemaliza. ngoja ntakuja na sehem soon itakuja

cc. Mentor
 

Aksante kwa jibu zuri, nasubiri sehemu b ya swali maana ndo niliona kuna utata namna ya kujibu mkuu ntamaholo
 

Mimi nimehama korogwe na kwamba barua kutoka kwa halmashauri niliyohamia ninayo hapa. Imeandikwa

Anwani ya mwandishi (Mkurugenzi-kulia)
tarehe (kulia)

kumb kumb na...
kwa Bw.......
Slp...
Korogwe. (kushoto)

Yah: KUKUBALIWA KUHAMIA HALMASHAURI YA....

Rejea kichwa cha habari hapo juu huku ukirejea barua yako ya tarehe....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…