Uandishi wa kweli wa Habari umekufa Tanzania (True Journalism has died in Tanzania)

Uandishi wa kweli wa Habari umekufa Tanzania (True Journalism has died in Tanzania)

A

Anonymous

Guest
Siku za karibuni tunazidi kuona upotovu wa ukweli kwenye Vyombo vya Habari unaozidi kukithiri nchini. Hii inatokana na Waandishi wa Habari za kiupelelezi kuangalia maslahi yao binafsi kwa kupokea hongo, na kuishia kuminya ukweli wa habari zinazotakiwa kutolewa.

Sijui niseme Waandishi wa Habari za kiupelelezi wengi walikuwa wanapenda na kuitumikia miaka ya nyuma wamekufa moyo kwasababu za kubanwa na Serikali au labda mambo kuwa magumu kiuchumi, ila siku hizi ukiwa na shida ukiweza kumpata Mwandishi wa kweli ambaye ataipika taarifa inayogusa pande mbili zenye mgogoro wa aina yoyote basi imekuwa ngumu, kwasababu ya Waandishi wengi kuangalia maslahi yalipo.

Naandika hii baada ya kutokewa na mgogoro kwenye mtaa ninaoishi. Nikatafuta Waandishi wa Habari ili hii habari ipate kuonekana na wanaohusika na lifanyiwe kazi.

Cha kushangaza Waandishi wa Habari kwanza wanataka hela yao ili waweke mfukoni, na mbaya zaidi waliwaruka walalamikaji kwa kwenda kwa mlalamikiwa na habari mzima ikaishia kubadilishwa, na walalamikaji wakaoneshwa wao ndio wabaya.

Hicho kitu kinauma sana jamani. Watu wanashida then wanaona labda wakienda kwa Waandishi wa Habari ili wasaidie malalamiko yao yapazwe Serikali ichukue hatua za kisheria hao Waandishi wanaishia kuwageuka walalamikaji na kuwafanya waonekane ni wabaya.

Soma Pia:
Tunahitaji Waandishi wanafanya kazi ya uandishi kwa kupenda kutoka moyoni, la sivyo tutaishia kuwa na habari zilizobadilishwa kwasababu ya maslahi binafsi ya Watu ambao ndio wanafanya maovu.

Waandishi wa Habari badilikeni, wananchi tunaumizwa, tusaidieni kupaza sauti zetu sisi wananchi tunaokandamizwa, na sio kutugeuka. kwasababu ya maslahi yenu binafsi.
 
Back
Top Bottom