“Uzinduzi wa kibao chenye namba za dharura kwa kila kaya.”
Hili ni pendekezo kwa Serikali ianzishe au iruhusu upachikaji wa ubao wenye orodha ya namba za dharura ndani ya nyumba kwa kila kaya lengo kuu la ubao huu ni “kutoa taarifa mapema kwenye mamlaka husika ili kupata msaada wa haraka na hitajika pale inapotokea ajari, hatari au viashiria vya uharifu.” Pia ubao huu wenye namba za dharura uwekwe kwenye maeneo maalumu kama vile kwenye vituo vya daladala, mabasi, kumbi za starehe na eneo maalumu lenye mkusanyiko wa watu wengi.
Ubao huu utasaidia kuhamasisha suala la utoaji wa taarifa kwani utakuwa “shawishi” kwa watu kuliko kuiweka kwenye simu ambapo mtu anaweza kuifuta au kusahau jinsi alivyoihifadhi lakini endapo utapachikwa eneo maalumu kama ukutani itakuwa vyepesi kwa mtu kutoa taarifa kwenye sehemu sahihi.
Ubao huu utasaidia jeshi la polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kutambua na kubaini maeneo hatarishi kwa raia endapo wananchi watautumia vizuri kwa kutoa taarifa mapema.
Ubao huu utaondoa woga kwa raia wanaoogopa kutoa taarifa juu ya tatizo lililojitokeza juu ya usalama wao kwani kupitia maongezi ya raia wengi yanabainisha wazi kuwa raia wengi uogopa kwenda kwenye vituo vya polisi na haita wafanya wapoteza muda wao kwani wengine hufanya hivyo kwa kutingwa na majukumu yao yanayowafanya wahisi kwenda kwenye vyombo vyenye kushughulika swala husika inaweza kutumia muda mwingi. Hili ubao huu uwe wa kudumu mamlaka husiki iweke na namba zisizo badilika.
NB: “Pia Ofisi za serikali nazo ziwe na ubao wa namba ya dharura au inayopokea kero ya mhitaji wa huduma aliyokutananayo ili kuboresha uwajibikaji” UBAO HUU WA NAMBA ZA DHARURA UENDE SAMBAMBA NA ELIMU YA UOKOAJI.
Nini maana ya elimu - Elimu ni mfumo wa urithishwaji wa maarifa kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.
Maana ya Maarifa - ni uwezo na ujuzi alionao mtu katika kutenda jambo fulani.
Nini maana ya uokoaji - Ni kitendo cha kutoa watu au vitu kutoka kwenye eneo la hatari au ajari.
UHUSIANO ULIOPO KATI YA ELIMU NA UOKOAJI
Katika kuhusianisha vitu hivi mtu aliyepata elimu anakuwa na maarifa na ujuzi, yaani uwezo wa kutenda jambo kwa ueledi zaidi kuliko mtu ambaye hana maarifa hayo ambaye anaweza kusababisha majanga makubwa zaidi katika kujiokoa mwenyewe au pale anapojaribu kutoa msaada wa kuokoa wengine. Hivyo mtu atakapokuwa na maarifa juu ya kuepuka hatari fulani au kutoa msaada kwenye hatari au ajali, elimu hii itapunguza athari zinazoweza kusababisha maafa makubwa.
Hii haina maana kwamba panapo tokea ajali basi mtu asuburi waokoaji wenye ubobezi huo kulingana na idara husika la hasha bali uwezo na ujuzi alionao umwezeshe kufanya uokoaji wenye tija kuliko maafa zaidi.
“ELIMU HII ITOLEWE KUANZIA SHULE ZA MSINGI/UPILI/VYUONI PIA NA KWA WANANCHI WOTE KUPITIA VIPINDI MBALIMBALI VYA REDIO, RUNINGA PAMOJA NA VYOMBO VINGINE VYA HABARI KAMA VILE MITANDAO YA KIJAMII”.
Elimu hii itolewe kwa kuzingatia pande mbili yaani upande wa wahanga wa ajari wafanye nini au wafuate hatua zipi pale watakapo kabiliwa na hatari au ajali. Pia Elimu hii itolewe kwa kumuangalia yule anayekuja kwa ajili ya kutoa huduma ya kwanza/ yaani kabla ya wataalamu waliobobea kufika eneo la tukio mtu huyu azingatie nini au afuate atua zipi anapokuwa kwenye kujaribu kutoa huo msaada.
BAADHI YA MATUKIO YA AJALI AMBAYO YAMEISHA IKUMBA NCHI YETU NA NINI KINGELIFANYIKA AU KIPI KIENDELEE KUFANYIKA
Meli MV Bukoba
Vita ya Idd Amini
Lori la Mafuta lililolipuka
Ajari ya ndege Mkoani Kagera
Mabomu ya Mbagala
Ajali za mabasi
Tetemeko la Ardhi
Uvamizi wa wanyamapori
“Kupitia elimu inayoandaliwa na idara husika mwananchi atambue ni eneo lipi la kujihifahi ikitokea vita, tetemeko la aridhi, milipuko ya mabomu, pia aelimishe ajiepushe na nini ili abaki kuwa salama kulingana na hatari au jambo lililomfika.”
MFANO
Kila baada ya taarifa ya habari, kila chombo cha habari kitoe elimu fupi juu ya suala zima la uokoaji au jinsi ya kuepuka hatari zaidi baada ya ajali kutokea. Mf “Ewe Mwananchi unapaswa kukaa umbali wa mita 50 au 100 kutoka kwenye eneo la tukio la ajali ya gari lililobeba nishati ya mafuta baada ya kuakikisha usalama wa dereva” na kisha kutoa taarifa kwenye namba iliyopo kwenye ubao wako wa namba ya dharura.
1. Polisi kwa ajili ya kuripoti uharifu.
2. Zimamoto kwa ajili ya kuripoti matukio ya moto.
3. Maafisa wanyamapori.
Kwa maeneo ya watu wanaoishi karibu mbuga za wanyama.
Ili waje haraka kutoa msaada wa kuwarudisha wanyama kwenye hifadhi kabla ya kuleta maafa makubwa.
4. Idara ya maji.
Mtu anaweza kujiuliza idara ya maji na uokoaji vinaingiliana vipi? Mitaani tumeshudia upasukaji wa mabomba ya maji, maji mengi yanapotea kihorela hivyo taarifa zitakapotolewa hayatapotea kihorela na kuhifadhi za ya kutumika kipindi cha ukame.
Sio tu mabomba ya maji hata pia tunashuhudia mifereji ya maji taka toka viwandani inapopata itirafu.
5.Tanesco kwa ajili ya itirafu mbalimbali za umeme.
Hii itasaidia kutoa taarifa mapema na kwa uharaka zaidi ili kurahisisha uokoaji katika kunusuru maisha ya watu na kupunguza uharibifu mkubwa yaani maafa makubwa.
PIA KUWEPO ELIMU TEMBEZI/ZIARA
Ninayoimani kuwa vipo vikosi vya uokoaji kulingana na vitengo mbalimbali, vikosi hivi vikitembelea mashuleni na vyuoni kwa ajili ya kutoa elimu suala hili litaleta tija sio kutembelea mashuleni na vyuoni tu, hata pia vikitembelea wanakijiji kwa ajili ya kutoa elimu mfano katika mikutano ya vijiji au hile ya adhara ninayo imani maeneo mengine yatafaidika na jambo hili hata pia suala la ulinzi kwa raia na mali zao unaweza kuimarishwa zaidi.
Elimu hii iwe endelevu kwenye vyombo vya kuhabarisha na isiwe inasubiri kutokea kwa ajari ndipo ianze kutolewa, hii itaongeza umakini zaidi na kuwafanya raia watunze kumbukumbu juu ya hatua za kufanya wakiona viashiria vya hatari au baada ya kutokea “Elimu hii isiwe ya kufunika kombe ili jambo lipite” katika kuonyesha uwajibikaji wa mamlaka husika bali tuone uwajibikaji huo kwa kuiendeleza elimu ya uokoaji.
Kupitia Elimu hii ya uokoaji na ubao huu wa namba za dharura “matukio ya Panya road yataisha”, “ vikundi vya uharifu vitaisha”. Tanzania itabaki kuwa sehemu salama na kisiwa cha Amani kwani taarifa sahihi naza mapema zinasaidia kwenye uokoaji wa majanga yanayotukumba kila mara na kupata msaada sahihi na wa haraka pale unapohitajika.

Upvote
3